HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 22, 2019

TIMU YA TAIFA YA WALEMAVU WA AKILI KUWASILI LEO

NA MWANDISHI WETU
TIMU ya Taifa ya walemavu wa akili, wanatarajia kuwasili nchini leo Machi 22 ikiwa na medali 15 kutoka katika michezo ya Dunia ya walemavu wa akili iliyomalizika Falme za Kiarabu (UAE).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays katika medali hizo, 12  za dhahabu, fedha moja na Shaba 2 zilizopatikana katika Riadha na Mpira wa Wavu.
Rays alisema michezo hiyo iliyochezwa UEA, michezo ya Riadha ilichezwa Abu Dhabi huku Mpira wa Wavu michezo hiyo ilifanyika Dubai.
Katika mpira wa Kikapu, Tanzania imeibuka mabingwa baada ya kuiadhibu Italia kwa seti 2-1 katika fainali.
Rays alisema katika riadha Tanzania imezoa medali 9 za dhahabu , Fedha moja na shaba 2 ambako Boniventura Anga wa Mtwara alipata medali ya dhahabu.
Aidha katika michezo hiyo, Tanzania ilishiriki michezo hiyo sambamba na wachezaji kutoka kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nyarugusu.
Katika mapokezi hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge anatarajia kuwapokea wanamichezo hao ambao wameiletea heshima Tanzania katika michezo hiyo.
Michezo ya dunia ya majira ya kiangazi yalianza Machi 14 na kumalizika Machi 21 (UAE).

No comments:

Post a Comment

Pages