Bondia
nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo akiwasili jijini Nairobi nchini
Kenya, tayari kwa pambano lake la Kimataifa dhidi ya bondia kutoka
Argentina, Eduardo Gonzalez litakalofanyika kesho Machi 23 mwaka huu.
(Na Mpiga Picha Wetu).
Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amewasili mjini, Nairobi
Kenya tayari kwa pambano lake la Kimataida dhidi ya bondia kutoka Argentina,
Eduardo Gonzalez lililopangwa kufanyika Machi 23 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Kenyatta (Kenyatta International Conference Centre).
Mwakinyo
kwa sasa ananoa makali yake chini kocha Tony Bellew kutoka Liverpool, Uingereza ambako alikuwa kambini chini
ya ufadhili wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.
Mbali
ya Mwakinyo, pia Bellew anamfundisha bondia Fatuma Zarika ambaye atapambana na
Catherine Phiri wa Zambia katika pambamo la ubingwa wa dunia wa uzito wa Super
Bantamweight wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC).
Mkurugenzi
wa Utawala na Udhibiti wa Kampuni ya Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema
kuwa bondia Mwakinyo atafanya
mazoezi chini ya kocha huyo chini ya uwezeshaji wa kampuni yao.
Tarimba
alisema kuwa mbali ya kampuni yao kuwezesha kambi ya Mwakinyo na Zarika, Pia
Bellew amevutiwa sana na viwango vya mabondia hao na wanaamini kuwa watafanya vizuri katika
pambano hilo.
Alisema
kuwa mabondia hao wamepata mafunzo bora na ya kisasa kutokana na umuhimu wa
pambano hilo.
“Wakiwa
mjini Liverpool, Mwakinyo na Zarika walijiandaa vyema kwa kuwa wanajua ugumu wa
mapambano yao. Kampuni ya SportPesa imeona umuhimu huo na lengo letu kubwa ni
kuona mabondia hao wanapata matokeo mazuri na kuwafurahisha wadau wa ngumi za
kulipwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Tarimba.
Alisema
kuwa Gonzalez atawasili Kenya kesho (Machi 20) ambapo Ijumaa (Machi 22)
mabondia wote hao watapima uzito kwenye hotel ya The Stanley.
Pia
mabondia hao watatembelea ofisi za SportPesa na kufanya mahojiano kwenye vituo
mbali mbali vya televisheni na redio mbali ya kula chakula cha jioni na
wafanyakazi wa kampuni yao.
No comments:
Post a Comment