HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2019

TBL yawapa shavu wanasoka Wanawake


Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli (katikati), Meneja Udhamini wa Kampuni ya Bia (TBL), David Tarimo na Balozi wa Castle Lager Africa nchini Tanzania, Ivo Mapunda, wakionyesha zawadi za washindi wa Bonanza la Wanawake mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Leaders. (Na Mpiga Picha Wetu).
 
 
NA MWANDISHI WETU
 
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Castle Lager, ilitangaza fainali za mashindano ya soka ya Wanawake ya Castle Lager 5 – Aside yatakayofanyika Aprili 20, 2019 katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager Pamela Kikuli, alisema kuwa, fainali za mashindano hayo zitashirikisha timu 16 kutoka kwenye vitongoji mbali mbali vya jijini Dar es Salaam.
 
Alisema, mashindano hayo ambayo yanafanyika hapa nchini kwa mara ya pili yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika ambapo, mwaka jana Tanzania ilishiriki katika mashindano hayo katika kiwango cha kimataifa nchini Zambia kwa upande wa Wanaume.
 
“Mwaka jana tuliyafanya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, huko Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia. 
“Kwa mwaka huu, tunatarajia kuwa na mashindano bora zaidi yatakayotusaidia kupata washindani na mabalozi wazuri katika michuano ya kimataifa,hivyo tumeona ni vyema tukashirikisha na Wanawake ili kuleta hamasa zaidi,” alisema Kikuli.
 
“Lengo ni kuwafikia wanywaji wa bia ya Castle Lager ikiwa ni pamoja na  kuwapa fursa ya kutimiza ndoto zao,” alisisitiza
Balozi wa Bia ya Castle Lager, Ivo Mapundaaliishukuru Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kupitia bia ya Castle Lager kwa  kuwashirikisha Wanawake mwaka huu kwani kwa kufanya hivyo mashindano yamwaka huu yatakuwa na msisimuko wa hali ya juu na kuwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi Viwanja vya Leaders kushuhudia fainali hizo.
 
Lakini pia, Balozi Mapunda alizitaja timu shiriki kuwa ni Chinga Queens kutoka Kariakoo, Siza Sisters kutoka Kariakaoo, Tabata Queens kutoka Tabata, Dragon kutoka Mwananyamala, Bulyaga kutoka Temeke, Mwangaza Queens (Temeke), Furaha Queens (Gerezani) na Umoja Queens (Kidongo Chekundu).
 
Nyingine ni  MRJ Queens (Mlandizi), Wema Dallas Queens (Mlandizi), Jupita (Buguruni) Sukita, Mercury kutoka Msimbazi, La Capilla Kutoka Mbagala, Santiago kutoka Mbagala, Girls Queens kutoka Msimbazi na Msimbazi Queens kutoka Msimbazi.
 
Nae Meneja Udhamini David Tarimo alizitaja zawadi za washindi kuwa Bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia Kikombe, Medali za Zahabu, Pesa taslimu Shilingi laki tisa pamoja na kuiwakilisha Nchi kwenye fainali za Kimataifa zinazotarajiwa kufanyika hapa Nchini.
 
Mwisho Kikuli aliwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo ambayo yatakuwa na burudani kutoka kwa Msanii wa Bongo fleva, Maua Sama pamoja na Dj. Kutoka E.A.Redio na RDJ Mammy

No comments:

Post a Comment

Pages