Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa, Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG), kwa Mkoa wa Mbeya namna mteja anavyoweza kutumia simu yake kufanya malipo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa, Dennis Sakia na anayefuatia ni Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Kadri Makongwa. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA FRANCIS DANDE
WATEJA wa Kampuni ya Tigo wa mikoa
ya Mbeya na Iringa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa kielektroniki
wa malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini
kwenye App yake ya Tigo Pesa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira jijini Mbeya (WSSA), Ofisa Uhusiano Msaidizi wa WSSA Mbeya, Kadri
Makongwa, alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya
malipo kwa wananchi.
Alisema kuwa mfumo huo umeleta
faida nyingi ikiwa ni pamoja na
kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na
kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali
“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa
wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo
kama Tigo.
Alisema wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka
ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka (WSSA).
Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na
kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya
mtandao.” alisema
“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha
kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Makongwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa Mbeya na Rukwa Ladislaus
Karlo, alisema zaidi ya wateja milioni 7
wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa, wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa
haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia
Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,”
Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo
Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika
la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka
ya Misitu (TFS) na Wizara ya Utalii.
Wadau wengine ni Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji
katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA),
Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na
idara nyingine zaidi ya 300.
No comments:
Post a Comment