Na Danson Kaijage, Handeni
CLEMENT Maganga mbaye ni
Mwakilishi wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Ten/Met amesema kuwa
mtandao wa elimu nchini imejiwekea malengo makuu matatu ya kuimarisha
elimu.
Akizungumza na wananchi,wadau
wa elimu pamoja na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho Wiki ya Elimu iliyofanyika kitaifa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga leo amesema kuwa
malengo hayo matatuni ni pamona na kuongeza uelewa kwa Umma juu ya haki
elimu iliyo bora.
Alitaja malengo mengine kuwa
ni kuhamasisha serikali kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama wenye
ulemavu,wito wa upatikanaji wa miundombinu na vifaa vya shule,mafunzo ya
walimu ikiwa ni pamoja na walimu wenye ulemavu.
Ameyataja malengo mengine kuwa ni pamoja na kuhamasisha na
kukumbusha jamii,Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuhusu
umuhimu wa uwajibikaji wa pamoja katika masuala ya Elimu na utekelezaji
wa malengo endelevi la nne na la Tano.
"Mkoa wa
Tanga hasa Wilaya ya Handeni kumechaguliwa kuwa sehemu ya kufanyia
maadhimisho kutokana na juhudi zanazofanywa na wilaya hasa katika upande
wa Elimu jumuishi"alieleza Clement.
Kwa upande
wa baadhi wanafunzi wa kike walisema kuwa wanakabiliana na changamoto
mbalimbali ya kukatisha masomo ikiwa ni pamoja na miundombinu kutokuwa
rafiki.
Wakizungumza na waandishi wa habari
wanafunzi hao wa kike walisema umbali wa kati ya shule na nyumbani
unachangia zaidi wanafunzi wa kike kurubuniwa na waendesha pikipiki
maarufu mama Bodaboda.
Hadija Omari ambaye ni
mwanafunzi wa kike alisema changamoto nyingine ambayo wanafunzi
wanatukana nayo ni pamoja na ukata unaotokana na familia zao kwa familia
kushindwa kuwapatia mahitaji wanayoyataka.
Naye
mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigera wakati akizindua maadhimisho ya
wiki ya Elimu Kitaifa wilayani Handeni alisema kuwa serikali inatambua
umuhimu wa asasi zisizokuwa za kiserikali zinavyokuza na kuhamasisha
umuhimu wa elimu na ubora wa Elimu nchini.
Shigera
alisema kuwa pamoja na mambo mengine mkoa umejiwekea marengo ya
kuifanya elimu kuwa shirikishi kwa jamii ili kuhamikisha inapandisha
kiwango cha ufaulu.
No comments:
Post a Comment