Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi jarida la Nchi Yetu
Tanzania, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) anayekipiga katika
Klabu ya KRC Genk ya Nchini Ublegiji Mbwana Samatta amara baada ya mazungumzo
baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jumanne (Mei 28, 2019)
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuliaji wa Timu ya
KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi
za Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) na Mshambuaji wa Kalbu ya KRC Genk ya Ubelgiji akifafanua jambo ka
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu
kulia) Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara
ya Habari (MAELEZO) leo Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta
Tours, Hamisi Waziri akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan
Abbasi wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO)
leo Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Nahodha wa Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha
ya pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuaji
wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji (katikati) mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO leo Jumanne (Mei
28, 2019) Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MAELEZO).
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO, DAR ES SALAAM
SERIKALI imesema itaendelea
kumsaidia kwa hali na mali Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
anayechezea Klabu ya Genk ya Nchini Ubelgiji Mbwana Samatta ili kuhakikisha
kuwa anafungua milango ya uwekezaji na kuiweka juu ramani ya Soka la Tanzania
katika anga la kimataifa.
Akizungumza leo Jumanne (Mei 28,
2019) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na Nahodha huyo waTaifa Stars,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbasi alisema Samatta ameonyesha njia iliyoshindwa kufikiwa na
wachezaji wengi wa miaka ya nyuma waliojaribu kucheza Soka la kulipwa katika vilabu
mbalimbali vya Nchi za Nje hususani Bara la Ulaya.
Dkt. Abbasi alisema Serikali
ilimteua Sammatta kuwa Balozi wake wa Utalii kutokana na sifa kubwa zilizoletwa
na mchezaji huyo nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa Serikali ina Imani naye
kubwa katika kufungua milango ya fursa za uwekezaji hususani katika miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano hapa nchini.
“Mbwana Samatta ameonyesha njia
ambayo ilikuwa ndoto iliyoshindwa kutimizwa na wachezaji wengi wa zamani, hatua
hii aliyofikia ni kubwa na imetokana na sifa kubwa ya nidhamu na kipaji cha
mchezo huu hili ni funzo kwa wachezaji wetu chipukizi” alisema Dkt. Abbasi.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema
kwa sasa yapo mambo makubwa na mazuri hususani vivutio vya sekta ya utalii,
hivyo kupitia nafasi yake ya Ubalozi Serikali itatoa msaada wowote unaohitajiwa
na mchezaji huyo ili kuhakikisha kuwa vivutio vya Tanzania vinabainishwa na
hivyo kutangaza mambo mazuri ya Tanzania.
Aidha Dkt. Abbasi alisema Ofisi
yake imeandaa mikakati mbalimbali ya mawasiliano ya kitaifa katika kuisema nchi
katika maeneo mbalimbali hivyo kumtaka mchezaji huyo kutumia majukwaa hayo kwa
ajili ya kuona namna bora ya kutumia fursa hizo ili kuitangaza Tanzania nje ya
mipaka yake.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alimtaka
mchezaji huyo kuwasiliana naye iwapo kutakuwepo na changamoto yoyote anayoweza
kuipata katika kutekeleza majukumu yake ya nafasi ya Ubalozi kwani kwa sasa
Serikali ya Awamu ya Tano imefungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa
ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua katika
kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Kwa upande wake, Nahodha huyo wa
Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema akiwa nchini Ubelgiji tayari amefanya
juhudi kubwa katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini,
ambapo mwanzoni mwa mwezi ujao madaktari 5 wa timu hiyo wanatarajia kuja nchini
kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini.
Samatta alisema raia wengi wa
kigeni wana shauku ya kutembelea Tanzania kutokana kusikia na kuona uzuri wa
vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Wanyama, hivyo akiwa Balozi wa Utalii afanya
kila liwezekanalo kukaa karibu na
viongozi na wachezaji wa klabu yake ya KRC Genk kuwaeleza uzuri wa Tanzania ili
na wao waonesha nia ya kuitembelea Tanzania.
“Wachezaji wengi hususani wale wa
kiafrika waliopo nje hususani Bara la Ulaya wanaipenda sana Tanzania, na hi
inatokana na sifa tuliyonayo, na hivyo kwa kutumia nafasi yangu ya Ubalozi
nitaendelea kushawishi waitembelee Tanzania” alisema Samatta.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamis Waziri aliishukuru Serikali kutokana
na jitihada mbalimbali inazofanya kwa ajili ya kuhamasisha sekta ya utalii
nchini na kusema taasisi hiyo itakuwa tayari kutangaza matukio mbalimbali kwa
ajili ya kulitangaza jina la Tanzania.
No comments:
Post a Comment