HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 21, 2019

NI SIMBA TENA 2018/19

Kikosi cha Simba.
 

NA JOHN MARWA


WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC, hatimaye wametawazwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL 2018/19), baada ya kuwajainisha Walina Alizeti Singida United kwa mabao 2-0, katika pambano lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.


Mabao ya Mnyarwada Medie Kagere ‘MK14’ dakika ya 9 na Nahodha John Bocco dakika ya 61, yameifanya Simba kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote baada ya kucheza mechi 36.


Simba walihitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kutwaa ubingwa kabla ya kuwavaa wageni wao, Miamba ya Soka kutoka Hispania, Sevilla waliotua nchini jana kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.


Ubingwa huo unakuwa wa 20 kwa Simba katika TPL, unaowafanya kuendelea kuwafukuzia watani zao ambao ndio mabingwa wa kihistoria hadi sasa, Yanga wakiwa wamelitwaa kombe hilo mara 27.


Ni dakika 3,240 zimetosha kwa Mnyama Simba kutetea ubingwa wa TPL walioutwaa msimu uliopita, wakisaliwa na dakika 180 kuhitimisha ligi msimu huu.


Michezo 36 imetosha kuwapa Simba uchampioni, wakishinda mechi 29, sare nne na kupoteza michezo miwili huku wakisaliwa na mingine miwili.


Simba imefanikiwa kufunga mabao 76 katika michezo hiyo 36, wastani wa kufunga mabao 2.1 kila mchezo, huku wakiruhusu mabao 14 sawa na wastani wa 0.8 kuruhusu bao kila mchezo.


Mnyama ameshinda michezo 17, pasipo kuruhusu bao huku ikitoa suluhu michezo minne Dhidi ya Yanga, Azam, Ndanda na Lipuli.


Katika mapambano waliyopoteza hadi sasa ni matatu dhidi ya Mbao FC walipolala 1-0 ungwe ya kwanza, Kagera Sugar michezo yote miwili, 2-1 na 1-0, huku wakifanikiwa kufunga bao moja pekee katika mechi walizopoteza na kuruhusu matatu.


Ni mechezo sita pekee ambayo kikosi cha Patrick Aussems kimeshindwa kupachika bao, minne waliotoka suluhu na miwili waliopoteza, huku wakifunga mabao katika michezo 30, 29 wakiibuka na pointi tatu huku mmoja wakipoteza.


Ubora wa kikosi chao, kimewafanya kuibuka mabingwa tena ukilinganisha na klabu zingine zinazoshiriki TPL msimu huu, wakifanya vizuri hata katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL), wakifika hatua ya Robo Fainali wakiondoshwa na TP Mazembe katika hatua hiyo.


Simba wanatwaa ubingwa wakiwa ndio timu iliyofunga mabao mengi kuliko timu zote msimu huu, wakifunga mabao 76, huku wakishikilia rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi wakiruhusu 14 hadi sasa.


Safu ya ushambuliaji ya Simba imekuwa bora hadi sasa, kwani Kagere anaongoza na mabao 23, Bocco 16 na Emmanuel Okwi 15, jumla yao ikiwa 54 kati ya 76 waliyofunga.


Mchezo wa jana ulikuwa wa aina yake, kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu, Simba wakizihitaji ili kutwaa ubingwa huku Singida wakihitaji kujiweka katika mazingira salama zaidi Ligi inapokwenda kufikia ukingoni.


Rekodi Mbaya waliyonayo Singida dhidi ya Mnyama, iliendelea kuwaadhibu kwani tangu watinge TPL hawajawahi kuokota hata sare kwa mabingwa hao.


Katika mechi nne za misimu miwili, Singida wamepoteza zote mbele ya Simba huku wakishindwa kufunga hata bao moja na kubugizwa jumla ya mabao 10, matano msimu wao kwanza na matano msimu huu.


Simba wanatwaa ubingwa huo kibabe wakitumia dakika 3,240, ambapo kila baada ya dakika 42 na sekunde sita wametikisa nyavu za wapinzani wao. Huku wakikubali nyavu zao kutikiswa kila baada ya dakika 231 na sekunde 43.


Mchezo mwingine wa TPL jana, Mbao FC ilikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Vijana wa Mjini, KMC kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.


Vikosi vilivyoanza jana, Singida United; Saidi Lubawa, Frank Zakaria, Gilbert Mwale, Salum Kipaga, Kennedy Juma, Rajab Zahir, Boniphace Maganga, Issa Makamba, Jonathan Daka, Habibu Kyombo na Geofrey Mwashiuya ‪


Simba; Deo Munishi ‘Dida’, Nicholaus Gyan, Mohamed Hussein, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, James Kotei, Haruna Niyonzima, John Bocco, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Mzamiru Yassin.

4 comments:

  1. alwɑyѕ i uѕed to rread smaller posts thaqt also clear theіr mоtive, and that іs
    also һappening with this paragraph which I am readіng at this time.

    ReplyDelete
  2. Ηello, i think hat i saᴡ yoս visited my web sitee sο i came to “return tһe faѵor”.I'm tryіng to find things to improve my weƅsite!I suppose itts ooк to uѕe a few of үoour ideas!!

    ReplyDelete
  3. I'm no longer sure wherе yoս're getting your information, but
    good topic. I must spend a while stսdying more or figuring out more.
    Thanks forr magnificent info I was оnn the lookout for
    this information for my misѕion.

    ReplyDelete
  4. Greɑt blog here! Additionally ypur site s᧐ muⅽh up very fast!

    What web host are you the use of? Can I am ցetting your assocіate
    һyperⅼink on your host? I desire my wweƅ site ⅼoaded up as fast as yours lol

    ReplyDelete

Pages