Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu nchini
kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na
kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka zao.
Mama Magufuli ametoa wito huo leo
tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa
ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.
Vyakula alivyotoa ni tani 5 za
mchele, tani 3 za sukari na tende. Hafla hiyoimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa
BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary
Kambwile na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.
Mama Magufuli pia amemuomba
Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote na kuwalipa malipo stahiki wakati wakitekeleza
moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.
“Kipindu cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia
na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.
Mama Magufuli amesema licha ya
kwamba Tanzania ina watu wa imani za Dini tofauti lakini siku zote wananchi
wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.
Ametoa mfano kuwa licha ya
tofauti za kidini zipo baadhi ya familia ambazo Baba Muislamu na Mama ni
Mkristo zinaishi kwa amani na kushirikiana katika masuala yote ya kifamilia na
kwamba sifa hii ni moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.
“Binafsi nakumbuka zamani nikiwa
mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe” ,
alisema na kuongezea: “Ni kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa
Watanzania , leo nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye
uhitaji…”
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiongea machache wakati
wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali
vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu Mkuu wa
BAKWATA Shekhe Nuhu Muma akitoa
shukurani wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi
mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu Mkuu
wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma msaada wa
vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji
jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 019.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Mkurugenzi wa
Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile
msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali
vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli katika picha ya kumbukumbu
na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu
Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na
wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa
msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi mmoja wa
wawakilishi msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi
mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019. (Picha na Ikulu).
No comments:
Post a Comment