HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 23, 2019

USAJILI WA BIASHARA UMEONGEZEKA KUTOKA MAKAMPUNI 62 KWA MWEZI HADI KUFIKIA 700-BRELLA


Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini(Brella) Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Afisa kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi  na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
 Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo  hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
 Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo  hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
Mwamko wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao.
 
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Brella Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Alisema hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika  ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni yatakayojisajili.
“Baada ya mfumo wa kutoka kwa vitambulisho vya Taifa na kutakiwa kutumia namba ya vitambulisho idadi ya makampuni yanayosajiliwa umeongezeka na kufikia idadi hiyo lakini bado tutaendelea kukutana na wadau kwa kutoa elimu kuweza kuongeza wigo mpaka “Alisema.
Aidha alisema malengo yao ni kuhakikisha wanapanua wigo mpaka na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo.
‘Usajili kabla ya mfumo ulikuwa ni mkubwa sana lakini ulikuwa unawagharmi wateja wetu kutokana na kwamba wengi walikuwa wakiibiwa na vishoka kwa sababu wanasafiri kutoka Tanga kwenda Dar kutokana na kwamba hapo awali kutokuwa na matawi na hivyo kupelekea kuingia gharama na kuwapelekea mzigo mkubwa hivyo kwa kuliona hilo tukatambulisha mfumo huo wa kusajili kupitia online na mwamko kabla ya mfumo na baada ya mfumo mwamko umekuwa mkubwa sana”Alisema.
Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi  na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
Alisema kwenye maeneo ambayo tayari wamepita mwamko  umekuwa mkubwa sana kutokana na wafanyabiashara kueleza namna ya mfumo huo unavyofanya kazi ikiwemo kukutana na maafisa biashara hivyo kuwa chachu ya ongezeko la usajili na uelewa umeongezeka sana.
Hata hivyo alisema baada ya kutoka mkoani Tanga wataekelea kwenye mikoa ya Kanda ya kaskazini mingine ikiwemo Kilimanjaro,Arusha na Manyara huku akitoa wito kwa watu watakaosikia wakala huo wapo kwenye mikoa yao watumie fursa hiyo kupata darasa ambalo litawapa uelewa mkubwa

No comments:

Post a Comment

Pages