Wachezaji wa Sevilla na Simba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mchezo wao wa kimataifa wa kirafika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa May 23, 2019. Picha na Aishi Manula on Instagram.
Beki wa Simba, Zana Coulibaly akiwania mpira na mchezaji wa Sevilla katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Sevilla ilishinda 5-4.
Mchezaji wa Sevilla ya Hispania akiwatoka wachezaji wa Simba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Sevilla imeshinda 5-4. Picha na TFF.
Wachezaji wa Simba wakipongezana katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba wakipongezana katika mchezo huo.
Beki wa Simba, Zana Coulibaly akiwatoka wachezaji wa Sevilla.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba Crescentius Magori, Mwakilishi wa Laliga barani Afrika, Antonio Barradas, Rais wa Sevilla Jose' Castro Carmona, Mkurugenzi wa wa Utawala wa Sportspesa, Tarimba Abbas na Rais wa TFF, Wallace Karia wakionyesha jezi za timu ya Sevilla wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea pambano lao la leo. litakalofanyika Uwanja wa Taifa. (Picha na Said Powa).
Wachezaji wa timu ya Sevilla ya nchini Hispania, wakiendesha Kliniki ya soka kwenye Uwanja wa Uhuru kwa vijana wa Kituo cha Michezo cha JK Park cha jijini Dar es Salaam. Timu hiyo iko nchini kwa ajili ya mambo mbalimbali ya kiufundi kwenye soka pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba unaopigwa leo jijini kwenye Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment