Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Anthony Mavunde, akipata maelezo kutoka kwa Robert Samson
kuhusiana na eneo ambalo amewekeza kufugia kuku. (Picha na Julieth Mkireri).
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akipata maelezo kutoka kwa Robert Samson
kuhusiana na eneo ambalo amewekeza kufugia kuku.
Na Julieth Mkireri, Kibaha
Na Julieth Mkireri, Kibaha
NAIBU Waziri Ofisi
ya Waziri mkuu,sera Bunge ,kazi,vijana ajira na walemavu Anthony
Mavunde ametaka vijana kuiga mfano wa wengine ambao wamekua wakibuni
mbinu za kujiajiri.
Mavunde
ametoa kauli hiyo baada ya kumtembelea mjasiriamali kijana Robert
Samson ambaye anatarajia kuanza ufugaji wa kuku katika eneo la Visiga
Madafu Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani
"Robert anaingia katika kundi la vijana wa mfano wanaojiajiri bila kusubiri ajira serikalini au sekta binafsi" alisema Malunde.
Alisema Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kuwawezesha vijana wanaojiajiri na kuwakwamua kiuchumi.
Akiongelea
kuhusiana na shughuli anazofanya kwasasa Robert alisema, pamoja na kuwa
na maduka makubwa ya nguo ameamua kutimiza ndoto take ya kufuga kuku.
Amewashauri vijana wengine kuiga mfano kwa kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira za serikalini.
Miundombinu
ya kufugia kuku hao ikikamilika anatarajia kufuga zaidi ya kuku 20,000
na kufungua vibanda katika maeneo mbalimbali hapa nchini kusambaza kuku.
No comments:
Post a Comment