Mkurugenzi wa NMB Bank, Albert Jonkergouw, akimkaribisha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwenye futari maalumu
iliyoandaliwa na NMB jijini Dodoma kwaajili ya wateja na wadau
mbalimbali. Kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,
akihutubia wageni mbalimbali waliohudhuria Futari iliyoandaliwa na NMB.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliw, akiwa katika picha ya kumbukumbu.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaja benki ya NMB
kuwa ni taasisi inayopaswa kuigwa kwa ubora wa huduma akisifia namna
walivyoweka mizizi katika maeneo ya vijijini ambako wengi hawajafika.
Majaliwa alitoa kauli hiyo juzi katika hoteli ya
New Dodoma wakati benki ya NMB ilipowakutanisha wadau kutoka mkoani hapa kwenye
futari maalum kwaajili ya Mwezi Mtukufu.
Waziri Mkuu alisema benki hiyo inaisaidia
serikali katika juhudi za maendeleo hasa katika kipindi hiki ambacho taifa
linaelekea katika uchumi wa kati hivyo anaomba Watanzania kwa Umoja wao
kudumisha, amani, upendo na mshikamano ili kufikia malengo.
Alisema serikali ambayo ina hisa ndani ya benki
hiyo, itaendelea kushirikiana nao pale wanapoona inafaa kufanya hivyo lakini
akawataka waendelee kuboresha zaidi huduma zao katika maeneo ambayo hawajafika.
“Siyo dhambi nikisema mnaongoza kwa kutoa huduma
bora, nawashukuru kwa kujikita katika taasisi kama mashule ambako mmesaidia
kupeleka madawati na vitabu, lakini nafurahi kusikia mmeanza kufadhili hadi
kwenye michezo, nawapeni hongera, tutaendelea kuwatia moyo na popote mlipo,”
alisema Majaliwa.
Katika ukaribisho wake, Mkurugenzi wa benki ya
NMB Albert Jonkergouw alisema benki hiyo inajishusha kwa kuwakumbuka waumini
katika kipindi hiki ambacho wanahitaji kuwa karibu na muumba wao hivyo
wanaungana katika tendo hilo jema.
Jonkergouw alisema wataendelea kufanya hivyo na
kufuata taratibu za huduma za fedha nyingi ikiwemo kuwasogezea zaidi huduma
watu ambao wamekuwa wakizitafuta kwa gharama lakini akasema katika futari
watahitimisha Mei 31 mkoani Tabora lakini kila mkoa wanatumia nafasi hiyo
kuwaalika na wawakilishi kutoka maeneo ya jirani.
No comments:
Post a Comment