Na Asha Mwakyonde
JAMII imetakiwa kuwa na mshikamano katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambayo yana tija kwa taifa.
Haya yalisemwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mwenezi wa Kata ya Kivule, Bihimba Mpaya (Chadema), wakati akichangia harambee ya ujenzi wa Kanisa la Waadventist wa Sabato lililopo katika kata hiyo alisema kuwa umoja ,Upendo na amani ndio ndio sifa ya Taifa letu.
Bihimba alisema kuwa ili kuwe na maendeleo katika jamii ni vema wanajamii wakashirikiana kwa lengo la kupiga hatua.
"Nimeguswa na ujenzi wa kanisa hili hivyo nimechangia mifuko 20 ya saruji katika harambee hii, kwani nyumba za ibadi hutumika kuliombea taifa amani,"alisema.
Aliongeza kuwa hata Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa kwenye nyumba ya mkiristo mwisilamu yupo na katika nyumba ya muislamu mkiristo yupo hivyo ubaguzu hauna nafasi katika taifa letu.
Naye Kaimu Mchungaji wa kanisa hilo Steve. Mbwambo alisema kuwa kwa sasa wanatumia kanisa dogo ambalo halikidhi mahitaji kutokana na wingi wa waumini.
Alisema kuwa lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 55, katika harambee hiyo ambayo waliwashirikisha viongozi mbalimbali wakiwami wa kidini,kisiasa na kiserekali ambapo walipata zaidi ya milioni 15.
" Kanisa hili litakuwa na uwezo wa kusaliwa na waumini 700 litakapokanilika," alisema Mchungaji Mbwambo.
Kwa upande wake muumini wa kanisa hilo ambaye pia ni mjumbe kamati ya ujenzi Claris Ager alisema kuwa wao kama waumini wanaona kuna haja ya kuwekeza katika ujenzi wa kanisa hilo kwani kufanya hivyo ni kujiwekea akiba kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment