Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku walipokutana jijini Dodoma Juni 10, 2019 wakati Butiku alipomtembelea kujadiliana mambo mablimbali
ikiwemo uzinduzi wa jengo la Mwalimu Nyerere lenye ukubwa wa ghorofa 30. (Picha
na Wizara ya Ardhi).
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi leo tarehe 10 Juni 2019 amekutana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku kujadiliana masuala
mbalimbali ikiwemo namna Wizara hiyo itakavyoshirikiana na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere katika maeneo yanayohusu wananchi.
Katika mazungumzo yao
yaliyofanyika Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma, Butiku alitumia
fursa ya kukutana na Waziri Lukuvi kumuelezea kazi za taasisi yake hasa katika
kushughulikia Amani, Umoja na Maendeleo ya watu.
Pia Mkurugenzi huyo wa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere alimueleza Lukuvi kuhusu ufunguzi wa Jengo la
Taasisi yake la Ghorofa 30 liliko Dar es Salaam ambalo linatarajiwa kufunguliwa
mwanzoni mwa mwezi Agosti 2019 ambapo
uzinduzi wake utaenda sambamba na sherehe za kumuenzi na kumbukumbu ya Baba wa
Taifa miaka 20 baada ya kifo chake.
Kwa mujibu wa Butiku wakati
wa ufunguzi wa jengo hilo pia kutafanyika Kongamano la Kimataifa kuhusu kazi za
Taasisi ya Mwalimu ikuhusisha Amani,Umoja na Maendeleo yenye tija kwa watu wote
huku msisitizo ukiwa katika utekelezaji wa sera ya kwenda katika nchi yetu.
Kupitia kikao hicho,
Butiku alipata ushauri kuhusu maeneo ambayo Taasisi ya Mwalimu Nyerere ingependa
hasa maeneo yanayohusu wananchi moja kwa moja vijijini na mijini na ambayo ni
muhimu kwa amani umoja na maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Waziri
Lukuvi alimshukuru Butiku kwa kumtembelea kwa lengo la kupata ushauri hasa
katika masuala yanayohusu wananchi na kueleza kuwa kikao chao mbali na
kubadilishana uzoefu lakini pia kililenga
katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo huku msisitizo ukiwa ni kuleta
Amani na Umoja kwa taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment