HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 23, 2019

MAONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA AFRIKA KUFIKIA KILELE CHAKE LEO NAIROBI NCHINI KENYA

Maafisa wa MSD Etty Kusiluka, Selwa Hamid na Doroth Mtatifikolo wakitoa maelezo kwa majaji wanaofanya tathmini ya maonesho ya Utumishi wa Umma Afrika,yanayofikia kilele chake leo mjini Nairobi, nchini Kenya.

Maonesho hayo ambayo yanashirikisha taasisi za serikali kutoka nchi mbalimbali Afrika yamelenga kuwasilisha ubunifu unaofanywa na taasisi hizo katika nyanja za Tehama na Utawala bora katika utoaji huduma.

MSD imewasilisha ubunifu wake kwa kuonesha mifumo yake miwili ya _Customer Porto na _Visitors management system_ inavyofanya kazi na faida zinazopatikana kutokana na kutumia mifumo hiyo miwili.

Mfumo wa _Customer Porto_ unamuwezesha mteja wa MSD kupata taarifa muhimu ambazo ni pamoja na upatikanaji wa dawa,bei za dawa, hatua ya maombi ya mteja, miamala ya wateja na fomu ya mteja ya kutoa mrejesho wa huduma anazopata.

Mfumo wa _Visitors Management System_ unarahisha kusajili wageni wanaingia MSD na kuweza kuwafuatilia na kuwasimamia kirahisi.

Washindi katika maonesho watatambuliwa na mgeni rasmi anayetarajiwa kuwa Rais wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta na kupata zawadi leo.

No comments:

Post a Comment

Pages