Mkurugenzi wa Aqua-Farms Organization Bw. Jerry Mang'ena akitoa neno la ufunguzi wakati wa kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani lililofanyika BUNI Hub jijini Dar es Salaam, ambapo maadhimisho hayo hufanyika kila ifikapo Juni 8 kila mwaka.
Mhe. Sware Semesi (MB) , (aliyesimama) akitoa salamu wakati wa kongamano maalum la Siku ya Bahari Duniani lililoandaliwa na Aqua-Farms Organization ambapo alisisitiza sera bora ni muhimu katika kuhakikisha kuna Malengo Endelevu katika kutunza na kulinda Bahari.
Bw. Kervin Robert Kutoka UNESCO Tanzania,akisoma ujumbe kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Audrey Azoulay kwa ajili ya Siku ya Bahari Duniani, alisema wanawake wanahusika sana katika maswala ya Bahari kwa malengo endelevu.
Afisa Mawasiliano wa Aqua-Farms Organization Bi. Nancy Iraba akisisitiza baadhi ya mambo muhimu kuhusiana na siku ya Bahari Duniani.
Dr Rosie Marie
Mwaipopo akielezea mambo mbalimbali yanayohusiana na utunzaji wa Bahari na
kusisitiza kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na utamaduni wa kulinda na
kutunza Bahari kwa maendeleo endelevu.
Katibu Mkuu wa Youngship Tanzania Bw. Gregory Mella Akitoa
mada fupi kuhusiana na maswala ya Bahari akihusisha na maswala ya jinsia wakati wa Siku
mdaharo wa siku ya Bahari Duniani.
Majadiliano yakiendelea
Mkurugenzi wa Aqua-Farms Organization Bw. Jerry Mang'ena akitoa neno la Shukurani baada ya kumaliza kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali kuzungumzia maswala ya Bahari.
Picha ya Pamoja baada ya Kongamano hilo muhimu la maswala ya bahari kukamilika.
No comments:
Post a Comment