HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 10, 2019

Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa

 Makamu Waziri wa Uholanzi Bi. Marjolijn Sonnema (watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega(watatu kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Teknolojia ya Maaabara ya kupima afya udongo kwa kutumia gari maalum uliofanyika Jijini Arusha hivi karibuni. kushoo ni Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Joroen Verheul, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT centre ltd Bw.Geoffrey Kirenga, wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na kulia ni Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dkt.Edmond Matafu ambaye ndie mwekezaji wa teknolojia hiyo nchini.
 Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dk. Edmond Matafu (kulia) akitoa maelekezo ya namna Maabara ya kupima afya ya udongo inavyofanya kazi kwa Makamu Waziri wa Uholanzi Bi.Marjolijn Sonnema(wapili kulia) mara baada ya kuzindua maabara hiyo inayotumia gari maalum hivi
karibuni jiijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Centre Ltd, Geoffrey Kirenga.
Gari Maalum yenye maabara ya kupima afya ya udongo limezinduliwa hvi karibuni jijini Arusha. Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) ndiyo itakayoendesha zoezi la kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima kote nchini kwa gharama ya shilingi 25,000 mpaka 30,000.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na Dk. Edmond Matafu, ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili na Usalama wa Chakula Bi. Marjolyn kutoka nchini Uholanzi, pamoja na Dk. Edmond Matafu, wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo. (Picha zote na Ahmed Mahmoud, Arusha).



Na Mwandsihi Wetu, Arusha

TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalumu lenye uwezo kupima zaidi ya sampuli 100 za udongo kwa siku moja limezinduliwa hapa nchini ili kupima udongo na kumhakikishia mkulima uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.

Uzinduzi wa Teknolojia hiyo kutoka nchini Uholanzi ulifanyika jijini Arusha kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega kwa niaba ya Tanzania na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Bi.Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kutoa teknolojia yake kwa Tanzania na kusema kuwa itasaidia kuleta mapinduzi katika uzalishaji mazao.

“Kupima afya ya udongo inatoa majibu juu ya ubora wa ardhi husika, mazao yanayofaa kulimwa katika eneo hilo, kiwango cha mbolea kinachotakiwa na kutoa makadirio ya kiwango cha mavuno katika eneo husika,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aliongezea kuwa gharama ya kupima shamba iliyowekwa ya shilingi 25,000 mpaka 30,000 wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapema mashamba yao kabla ya kufanya kilimo ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake na nini afanye ili tija ya uzalishaji iongezeke.

“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tunakila sababu ya kuhamasisha wakulima nchini kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao lilalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha ili aweze kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema.

Naibu Waziri Ulega aliesema kuwa mageuzi katika sekta ya kilimo yatapatikana kupitia teknolojia hii ya kupima afya ya udongo na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo hali itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongezea thamani ya mazao.

“Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kunachochea kasi ya maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi mbalimbali katika kuiletea nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) kwa kuwekeza kwenye ketnolojia hii,” alisema Ulega Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dkt.Edmond Matafu alisema magari manne yapo tayari pamoja na handheld soil scanner 100 ambazo zitatumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya kuchukua sampuli za udongo katika maeneo ya vijiji kote nchini.

“Hii itasaidia kufanya zoezi la kupima afya ya udongo kwa wakati pasipo kuchelewa kipindi cha kulima ambapo itampa unafuu mkulima kujua mahitaji katika shamba lake ili aweze kupata tija katika uzalishaji mazao,” alisema Dkt. Matafu.

Aliongezea kuwa juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kati na viwanda zitatekelezeka kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa ili maendeleo tunayoyatarajia yaweze kufikiwa kwa vitendo.

“Zoezi la kupima afya ya udongo litafanyika kote nchini kwani tumejipanga vizuri katika kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo ushirikiano ndio kitu muhimu katika kufanikisha zoezi hili ambalo litakwenda kuinua hali ya uzalishaji zao nchini,” alisema Dkt. Matafu.

Uzinduzi wa Maabara ya kupima udongo kwa kutumia gari maalum ulishuhudiwa na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania

Joroen Verheul, Katibu Mkuu Wizara ya Mifungo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini, Bw. Geoffrey Kirenga.

1 comment:

  1. Habar naitwa Mussa nipo Mbarali Mbeya naomba mawasiliano ya jinsi ya kupata huduma hiyo ya upimaji wa udongo ili nipime shamba langu la mpunga

    ReplyDelete

Pages