Na Suleiman Msuya
MADIWANI
na watumishi wa Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro wamesema
watatenga bajeti ili kupima vijiji na kuendeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi
katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) katika vijiji vipya.
Wawakilishi
hao wa wananchi wametoa ahadi hiyo wakati wakifanya maazimio ya mkutano
uliondaliwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG),
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa
Misitu Tanzania
(Mjumita), Shirika la Kuendeleza Nishati Asili (TaTEDO) chini ya
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi ((SDC).
Diwani
wa Kata ya Mukulazi wilayani Morogoro, Abeid Muyanga alisema mradi huo
ni fursa ambayo haifai kuachwa kuendelezwa hivyo kuwata wataalam wa
wilaya kushirikiana na wataalam wa TTCS kuendeleza kwa vijiji vipya.
Mukulazi alisema maendeleo yanahitaji ushirikiano zaidi hivyo ni vema madiwani wakashikamana wakati mradi ukielekea ukingoni.
"Kwa
kweli miaka miwili na nusu ya uwepo wa mradi huu imekuwa ya mapinduzi
kwa kila sekta hivyo ili kuepusha kurudi nyuma tunapaswa kushikamana na
kuendeleza," alisema.
Kwa
upande wake Diwani wa Tununguo, Ndonga wa Ndonga alisema mradi huo
umesaidia miradi mingi ya maendeleo hivyo hakuna budi kuindeleza kwa
ushirikiano.
"Kwangu
Mlilingwa huduma za maji, umeme, afya, elimu na huduma nyingine
zimeboreka na sababu kubwa ni USM kupitia mfumo wa TTCS," alisema.
Akichangia
katika mkutano huo Diwani wa Kolelo Eridius Mbena alisema dhana ya
Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) ni ya kuungwa mkono na viongozi
ambao vijiji vyao vina misitu hasa ya miombo.
Mbena
alisema vijiji vitano ambavyo vipo kwenye mradi wa TTCS umefanikiwa
kuleta mageuzi hivyo wao wanawajibu wa kuunga mkono na kuendeleza.
"Mimi
nitapambana kuhakikisha mradi huo unaendelea lakini pia naomba
tupambane vijiji vipimwe kwani vila kuingia katika mpango wa matumizi
bora ya ardhi hatuwezi kufanikiwa," alisema.
Diwani
wa Konde, Clara Laurence alisema vijiji vya kata yake havina misitu ya
miombo ila vinaweza kutumia mfumo huo katika uvunaji wa mbao na kuwa na
matokeo chanya.
"Kule
kwangu miombo haipo lakini misitu ipo nadhani mfumo huu unapaswa
kupelekwa ili kutumika katika uvunaji wa mazao mengine," alisema.
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Kibena Kingo alisema katika kuonesha wamedhamiria
kuendeleza halmashauri imekubaliana kutumia Msitu wa Sesenga Lumbachini
kuanza mradi kama huo.
Kingo
alisema ili kufanikisha dhamira hiyo ni jukumu la madiwani kushikamana
kwa kuhakikisha fedha zinatengwa na kutumika eneo husika.
Wakuu
wa Idara ya Ardhi na Maliasili, Wahida Beleko, Asenga Christopher Ofisa
Misitu, Idd Ndabhona Mwanasheria na wengine walisema wapo tayari
kushirikiana na madiwani kuendeleza miradi ya USM vijijini
No comments:
Post a Comment