Na Kenneth Ngelesi, Rungwe
MADIWANI
Halmashauri ya Rungwe Mkoani wameagiza Ofisi ya Mkurugenzi kuharakisha
usambazi wa mipira ya kiume ‘Kondomu” katika Vituo vya Afya, Zahanati na
maeneo ya vijijini kwani imeadimini na hivyo kuhatarisha maisha ya
wananchi.
Akizungumza
katika kikao cha baraza la madiwani kilicho keti juzi Diwani Samwel
Mwakasege kata ya Matwebe alisema kuwa katika kata yake huduma hiyo
imeadimika hivyo anaiombo Ofisi ya Mkurugenzi ifanye haraka kusambaza
mipira hiyo.
Mwakasege
alisema ni vema ofisi ya mkugenzi kupitia Mganga Mkuu ikaharakisha
kusambaza mipira hiyo kwani maeneo mengi hazipo na hata zikipiatikana
zinauzwa kwa bei kubwa kuanzia 1500-2000 na wananchi wengi hawawezi
kumudu.
‘Mwenyekiti
kwenye Vituo vya Afya Zahati kondomu hakuna, niiombe Ofisi ya
Mkurugenzi iharakishe kusambaza mipira ya kiume maana watu wetu maisha
yao yapo haratini zinazopatiakana zinauzwa bei kubwa na wananchi wetu
hawawezi kumudu bei gharama’ alisema Mwakasege.
Akitolea
ufafanuzi juu kuadimini kwa kondomu katika Zahanati na vituo vya Afya
kwa niaba ya Mkugenzi wa Halmashauri, MgangaRungwe na Mganga Mkuu Wilaya, Dk John Damian Mrina alisema wamepotekea ombi suala hilo kutoka kwa Diwani na watalifanyia kazi.
Dk
Mrina alisema Mipra ya kiueme ipo ya kutosha kwana mpaka Mei 7 mwaka
huu kwenye ghala la dawa kuna mpira zaidi ya 50,000 hivyo wanashukuru
kwa taarifa hivyo wataifanyia kazi.
‘Mwenyekiti
Mzigo upo wa kutosha kwani nimewasiliana na mtu dawa kwamba mapaka jana
kuna kondomuy zaidi ya 50000 hivyo niwatoe shaka wahesmiwa madiwani
ommbi lao tutalitekeleza na maalia ambapo hazipo tutawasiliana na
waganga wakuu katika Vituo vya Afya na Zahanati’ alisema Dk. Mrina.
Akihitimisha
hoja hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ameitaka ofisi ya Mkurugenzi
kuharakisha kusambaza mipira haraka katika vituo vya Afya
Zahanati,kwenye baa na vilabu vya Pombe za kienyeji ili kunusuru maisha
ya wananchi.
‘Mkurugenzi
naomba mfanye haraka kusambaza kondomu kwenye vituo vya Afya, Zahanati
lakini kwenye vilabu vya pombe za kienyeji ndiko waliko wananchi, narudia hasa kwenye vilabu vya pombe chonde watu wetu wataangamia’alisema Mwakota.
No comments:
Post a Comment