Mtafiti Kiongozi Dk. Gration Rwegasira, akiwasilisha ripoti ya utafiti kuhusu athari za Viwavijeshi Vamizi kwenye mazao, mkoani Dodoma juzi. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Suleiman Msuya
Na Suleiman Msuya
WATAFI
wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na wadau
wengine wa kilimo wamebaini Viwavijeshi Vamizi vimeathiri mazao katika
mikoa 21 nchini.
Utafiti
huo umefanywa kwa kipindi cha miezi minne kwa ufadhili wa Shirika la
Chakula Duniani (FAO) ambapo wilaya 42 katika mikoa 21 zilihusika.
Mtafiti
Kiongozi kutoka SUA, Dk. Gration Rwegasira alisema wamelazimika kufanya
utafiti huo ili kuweza kubaini athari za wadudu hao hatari kwenye
kilimo.
Alisema mikoa na
wilaya ambazo wamepita athari ni zaidi ya asilimia 80 hivyo nidhahiri
kuwa mavuno hayatakuwepo kwa wakulima wa mikoa husika.
Mtafiti
huyo alisema jitihada zaidi zinahitajika kukabiliana na viwavijeshi
hasa kwa kutoa elimu kwa maofisa ugani na wakulima kuwatambua na
kukabiliana nao.
Rwegasira
alisema ripoti hiyo ya utafiti amesema usalama wa chakula sio ukubwa wa
eneo lililolimwa pekee bali kile kinachovunwa na wakulima ndicho
kinachoweza kuonyesha kwamba nchi inajitosheleza kwa chakula.
"Tumezunguka
kwa takribani miezi minne kipindi hiki cha kilimo na mavuno hali sio
nzuri Viwavijeshi Vamizi vimeharibu mazao kwa zaidi ya asilimia 80 na
ukiangalia kwa kina tatizo ni uelewa wa maofisa ugani na wakulima kuhusu
kukabiliana na hali hiyo," alisema.
Alisema
katika utafiti wao wamebainisha kuwa kuna matumizi makubwa ya madawa ya
viwandani yaani viuatilifu katika kumdhibiti mdudu huyu bila mafanikio
na hivyo kuhatarisha afya ya wakulima na mazingira.
Aliongeza
kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa viuatilifu wasio waaminifu wamekuwa
wakiwauzia wakulima dawa za kunguni na kwakuwa wakulima hawajui na wapo
kwenye taharuki ya kuokoa mazao yao yanateketea wananunua na kwenda
kupulizia bila mafanikio.
Dk. Rwegasira
alisema wakulima baada ya kuona viuatilifu hivyo havifanyi kazi baadhi
wanachanganya kiuatilifu zaidi ya kimoja bila kujua athari za kikemikali
za mchanganyiko wa madawa wanayochanganya.
Kiongozi
huyo wa utafiti huo kutoka SUA alisema tatizo kubwa linatokana na
maafisa ugani wenyewe ambao ndio wanaotakiwa kumshauri mkulima kukosa
elimu ya utambuzi na udhibiti wa mdudu huyo na wala njia bora za
kumkabili na hivyo kuendelea kusababisha athari kwenye mashamba ya
wakulima.
"Utafiti huo
umebaini kuwa athari za wadudu hao zinetofautiana katika eneo moja la
kiikolojia na lingine na kwamba sehemu zenye mvua nyingi mashambulizi
hayakuwa mengi kama ilivyo kwenye maeneo yanayopata mvua kidogo ambapo
mvua zimechangia Kuwaua," alisema.
Alisema
athari za mashambulizi yalikuwa kati ya asilimia 30 hadi 100 kasoro
kwenye mikoa ya Njombe,Mbeya na Iringa ambapo yalikuwa asilimia 15.
Dk. alisema
mashambulizi yalikuwa makubwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kusini,
Mashariki na Rukwa na hivyo kuathiri sana mashamba ya wakulima.
Aliitaja
baadhi ya mikoa iliyoathirika na Viwavijeshi Vamizi kuwa ni Iringa,
Mbeya, Njombe, Arusha, Kilimanjaro, Simiyu, Geita, Kagera, Tanga,
Manyara, Lindi, Mara, Mwanza, Katavi, Rukwa, Morogoro, Singida, Tabora
na Songwe.
Rwegasira
alisema swala la aina ya mbegu hali kuonyesha tofauti ya mashambulizi
kati ya mbegu za asili na chotara maana mashamba yote yaliathiriwa
sawasawa bila kujali aina ya mbegu walizotumia hasa baada ya baadhi ya
wakulima kusema mbegu za asili hazishambuliwi.
No comments:
Post a Comment