Mhandisi Burton Komba (wanne kulia), anayesimamia mradi wa ujenzi wa
Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA-TB3), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani
nchini, Hamad Masauni (mwenye suti)
alipotembelea jengo hilo hivi karibuni.
Afisa Usalama Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Ramadhani Mkumbukwa (aliyenyoosha mkono), akimweleza Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wapili kulia) namna ya ukaguzi wa
abiria na mizigo unavyofanyika wakiwa kwenye jengo la tatu la abiria la
JNIA hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (mwenye suti), akionyesha
jambo akiwa kwenye eneo la ukaguzi wa abiria na mizigo wakati alipotembelea
jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius
Nyerere (JNIA TB3) hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (kulia) akiongozana na
maafisa wa ulinzi na usalama kukagua sehemu za kupitisha mizigo kwenye
Jengo la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa la Julius Nyerere (JNIA
TB3), alipofanya ziara hivi karibuni.
Na
Mwandishi Wetu
Wizara
ya Mambo ya Ndani nchini, itaongeza askari watu na mbwa kwa ajili ya kuimarisha
ulinzi na usalama kwenye viwanja vya Ndege nchini.
Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi
katika Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA TB3).
Masauni
amesema serikali inatarajia kuongeza askari mbwa wengi wenye mafunzo na sifa, ili
kuongeza ufanisi na ulinzi wa viwanja vyote vya ndege.
“Idadi
ya mbwa inatakiwa iongezwe hasa inapokaribia kuhamia kwenye jengo jipya la tatu
la abiria, ambalo litakuwa na idadi kubwa ya abiria na changamoto nyingi, pia
kwa viwanja vingine navyo vitaangaliwa kwa suala la ulinzi,” alisema Masauni.
Hata hivyo,
amesema hatasita kukifuta kitengo cha mbwa endapo hakutakuwa na mbwa wa kukidhi
mahitaji na wenye sifa zote, kwani kwa sasa askari binadamu ni wengi zaidi.
Ametoa
maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),
Simon Sirro kuhakikisha mfumo na ushiriki
wa askari wake unaweza kuboreshwa na wale wanapelekwa viwanja vya ndege wawe na
sifa na vigezo maalum vya kuweze kubaini vitu kama nyara za serikali, madini na
madawa ya kulevyia.
“Hii
itasaidia kwa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika udhibiti, jingine
ni kuhakikisha IGP analisimamia na kulitekeleza kwa haraka sana, kwani tumekuwa
na askari mbwa waliopata mafunzo maalum ya kubaini vitu mbalimbali
vinavyopitishwa kwenye viwanja vya ndege, hivyo maelekezo yangu kwake tuongeze
idadi ya mbwa wenye sifa hapa JNIA ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema
Masauni.
Masauni
amefanya ziara hiyo siku moja baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kushughudia makabidhiano ya kilo 35.267 za
dhahabu zilizokamatwa Februari 15, 2019 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment