HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2019

TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Bukoba katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wananchi wakipata huduma katika banda Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA.
Mwananchi akitoa maelezo katika fomu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Bukoba.
Wananchi wakisoma kitabu cha Muongozo cha TCRA.
Mkuu wa Kitengo wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA, Thadayo Ringo akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada wilayani Bukoba.
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi, akizungumza katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kushirikiana na wadau Wilayani Bukoba mkoani Kagera.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas William akizungumza na wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA wilayani Bukoba.


Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Wakazi wa Bukoba mkoani Kagera na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Meneja wa Kanda ya Ziwa  wa TCRA, Francis Mihayo,  amesema ni fursa kwa wananchi wa Bukoba kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano.

Mihayo amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

"TCRA iko karibu na wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Mihayo

No comments:

Post a Comment

Pages