HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 24, 2019

VIPAJI VYA KUIMBA KUTAFUTWA

NA DENIS MLOWE, IRINGA

MASHINDANO ya kutafuta vipaji vya kuimba yanatarajia kuanza hivi karibuni katika kata ya Mwangata kwa vijana mbalimbali kutoka kata kuonyesha vipaji vyao. 

Akizungumza na Tanzania Daima, Diwani wa Kata ya Mwangata, Nguvu Chengula (pichani), alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika Ukumbi wa shule ya Sun Academy ambapo amewataka vijana wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi. 

Nguvu ambaye hivi karibuni alianzisha mashindano ya mpira ya kombe la Nguvu na ubingwa kuchukuliwa na Isoka fc alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuibua vipaji katika kata hiyo. 

Alisema kuwa katika kata ya Mwangata kuna vipaji mbalimbali baada ya kubaini wakati wa mashindano ya mpira na kuombwa na vijana hao kuanzisha mashindano ya kutafuta vipaji. 

"Natoa wito kwa vijana wa kata ya Mwangata kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya ya kuimba kwa kuwa tumejipanga vyema na kikubwa wapige simu kwa namba 0657497294 ambaye ni mratibu wa kutafuta vipaji" Alisema

Nguvu alisema kuwa kata ya Mwangata hapo mwanzo ilikuwa haina mwamko katika tasnia mbalimbali za michezo hivyo tangu awe diwani mwamko umekuwa mkubwa kwa kutumia msemo wa yajayo yanafurahisha.

Alisema kuwa licha ya mashindano ya kutafuta vipaji amepanga kuanzisha mashindano mengine ya soka yatakayojulikana kwa jina la Mtaa kwa Mtaa Challenge Cup ambayo yatashirikisha timu za mitaa yote ya Mwangata. 

Nguvu ambaye amejitokeza mmoja ya wadau ambao wameinua michezo mkoani hapa alisema washindi wa mashindano hayo watarajie zawadi nono kuliko zilizotolewa katika kutafuta bingwa wa kombe la Nguvu.

Katika mashindano yaliyoisha hivi karibuni ya Nguvu Cup bingwa aliondoka na sh. 500000,mshindi wa pili sh. 300000 na mshindi wa tatu sh. 200000.

No comments:

Post a Comment

Pages