Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (wa nne kushoto), akifurahi jambo na madiwani wa Halmashauri ya Muheza na viongozi wa wilaya hiyo katika ufunguzi wa Ligi ya Adadi Cup juzi katika Tarafa ya Bwembwera ambapo timu 14 zimeshiriki ligi hiyo. (Picha na Steven William).
Na Steven William, MUHEZA
LIGI ya mpira wa miguu ya Adadi CUP imeanza kutimua vumbi tena kwa mara ya nne katika Tarafa ya Bwembwera wilayani Muheza mkoani Tanga kwa kukutanisha timu 14 kutoka katika tarafa hiyo ya Bwembwera.
Ligi hiyo ya Adadi CUP ambayo imedhaminiwa na mbunge wa jimbo la Muheza balozi Adadi Rajabu imezinduliwa juzi jioni katika kiwanja cha kuchezea mpira cha kijiji cha Songa batini kata ya Songa wilayani Muheza ambapo mgeni rasmi alikuwa mbunge wa jimbo la Muheza Adadi Rajabu ambae alifuatana na katibu wa CCM wilaya hiyo Mohamed Moyo na
madiwani.
Katika ligi hiyo zimeshirikishwa timu kutoka katika kata ya
Tongwe,Kata ya Nkumba,Kata ya Potwe,Kata ya Kwafungo,Kata ya Songa na Kata ya Mhamba ambazo zitaanza kutimua vumbi katika vituo viwili ambapo ni kata ya Songa na kata ya Tongwe.
Ufunguzi wa ligi hiyo uliyofanyika katika kiwanja cha kuchezea mpira cha kijiji cha Songa batini walicheza timu ya Songa FC na timu ya Tongwe FC ambao mashabiki wa soka walifurika katika uwanja huo.
Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hizo mbunge huyo alisema kuwa ameanzisha ligi hiyo katika Tarafa zote nne za wilaya ya Muheza kwa lengo la kusaka vipaji vya vijana katika wilaya hiyo kwani hivi sasa mpira ni ajira.
Mbunge huyo alisema kuwa katika ligi hizo washindi wamekuwa wakipewa zawadi ya fedha,Ng'ombe,Jezi,Mbuzi, kikombe na Mipira ili lengo kubwa kutoa motisha katika timu hizo zilizoingia fainali.
Alisema kuwa kutokana na kuanzisha ligi hizo tayari kuna vijana wameshachukulia na timu kubwa ikiwamo Yanga,Costal Union,Simba na K MC ya Kinondoni jijini Dar ambapo wamepata ajira.
Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo alisema kuwa kuanzisha ligi hizo za Tarafa katika wilaya ya Muheza kutawezesha vijana kukuza vipaji.
Alisema kuwa serikali itahakikisha inapitia maeneo yote yaliyotengwa kwa jili ya viwanja vya michezo kama kuna watu wamejenga basi serikali itawachukulia hatua kali za kisheria na kuchukuliwa maeneo hayo kurudi
serikalini.
Moyo aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kuunda vikundi kwa ajili ya kupata mkopo wa fedha kutoka halmashauri ya wilaya ya Muheza ile asilimia kumi lengo ni kuhakikisha vijana wanajiendeleza katika maisha na sio
kuishia kulalamika serikali mbaya haiwasaidii kitu.
No comments:
Post a Comment