HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

August 16, 2019

Chuo Kikuu Mzumbe yasaidia majeruhi wa moto Moro

Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma (wa pili kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. (Picha na Francis Dande).
Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma (kulia), akiwaongoza watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na wanafunzi wa chuo hicho Kampasi ya Dar es Salalaam.
 Vifaa tiba tiba vikishushwa.
Makabidhiano ya vifaa tiba.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Prosper Ngowi (katikati), akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma, kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam.

Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma, akizungumza baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. 
 Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma, akimshukuru Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Prosper Ngowi, baada ya kupokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Prosper Ngowi (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa wa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam.

 Picha ya pamoja.
 Asanteni sana....Dk Deus Buma (kulia), akimshukuru Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
 Kukabidhi nyaraka.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Wilson Magembe, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba.

NA MWANDISHI WETU

CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kimetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Prosper Ngowi, alisema kuwa msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 1. umetokana na kuguswa kwa wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho.

“Kwa kutambua mahitaji ya majeruhi hao, wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam tumeguswa sana. Kama sehemu ya wajibu wetu katika kusaidia jamii, tumechangia damu pamoja na kununua vifaa tiba mbalimbali ambavyo tunavikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu,” alisema Prof. Ngowi.

Alibainisha kuwa, vifaa hivyo vimenunuliwa kutokana na michango ya wafanyakazi na wanafunzi wa Kampasi ya Dar Es Salaam na kwamba msukumo umetokana na kutambua mahitaji ya majeruhi hao katika kupata matibabu yao.

Aidha Prof. Ngowi aliongeza kuwa kutoa na kurudisha kwa jamii ni sehemu ya mpango mkakati wa chuo hicho na  kuwataka wadau wengine kujitokeza ili kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali hiyo wanaoendelea kupata matibabu.

“Tunaendelea kuwaombea majeruhi waweze kupona na kurejea katika shughuli zao za ujenzi wa taifa. Kwa waliofariki tunamwomba Mungu azipokee roho zao. Kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na janga hili kwa namna moja au nyingine tunawapa pole sana na tunamwomba Mwenyezi Mungu awape wepesi,” aliongeza

Akipokea msaada huo, Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma, alisema: “Msaada huu utafaa kwa wagonjwa wa majeraha ya moto, kwa sababu vifaa hivyo ndivyo vinavyohitajika, kwani Pure Glycerine na Petroleum Jelly ndio vinavyotumika katika kutengenezea wa blanketi kwa ajili ya kufuniki vidonda vyao.

No comments:

Post a Comment

Pages