MKUTANO WA KILELE WA SADC MUBASHARA DStv KUPITIA TBC
Chaneli
ya TBC ya Tanzania kuonekana katika nchi za SADC ili kuwawezesha
wananchi wa nchi hizo kushuhudia mubashara mkutano wa Kilele wa 39 wa
SADC
Dar es Salaam, Tanzania; 16 August 2019
– Katika kuhakikisha
kuwa wateja wake wanafuatilia habari za mambo yote muhimu yanayowahusu,
MultiChoice Africa imeamua kuonyesha mubashara Mkutano wa kilele wa 39
wa SADC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam. Kwa uamuzi huu, wateja
wa DStv katika nchi za SADC sasa wanashuhudia maendeleo ya mkutano huo
mubashara kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania – TBC.
DStv
sasa imefungua chaneli ya TBC kwenye soko lake la SADC kwa siku tatu
kuanzia 16 Agosti hadi 19 Agosti 2019 ambapo wateja wote wa DStv katika
nchi hizo wataishuhudia
TBC kupitia DStv Chaneli 199 na hivyo kufuatilia moja kwa moja
yanayojiri katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema kuwa kutokana
na uhusiano mzuri na Serikali ya Tanzania,
na kwa kuzingatia uzito wa mkutano huu unaofanyika hapa nchini kwetu,
MultiChoice imeamua kutenga chaneli maalum kwa nchi za kusini mwa Africa
ili kuwezesha kurushwa mubashara kwa matangazo ya mkutano huo kupitia
chaneli yetu ya Taifa – TBC. “Kwa kuwa tuna
mtandao mkubwa kote barani Afrika tumeamua kwa makusudi kabisa
kushirikiana na shirika letu la utangazaji TBC kurusha mubashara
matangazo haya katika nchi zetu za SADC”
“Uamuzi
huu ni ushahidi tosha kuwa ushirikiano wetu na serikali kupitia TBC
umeleta matunda makubwa kwani hivi sasa mamilioni
ya watu katika nchi za SADC wanaweza kushuhudia mubashara tukio hili
muhimu. Hii ni sifa kubwa kwa nchi yetu” alisisitiza Jacqueline.
Kwa
upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbasi, amesema kuwa
Serikali kupitia TBC ambayo inarusha mubashara mkutano huo muhimu
inafurahi kuona
kuwa kwa kushirikiana na wadau imefanikisha kuoneshwa kwa mkutano huo
katika nchi zote za SADC kupitia TBC ndani ya DStv.
Mkutano
kama huu hufanyika mara moja kila mwaka na unahusisha wakuu wa nchi
wanachama na hujadili masuala ya msingi kuhusu ustawi na maendeleo ya
nchi wanachama.
Chaneli
hiyo maalum ya DStv ambayo itaonyesha TBC kwa nchi za Kusini mwa Africa
itaonekana kupitia DStv 199 na itaonekana katika vifurushi vyote vya
DStv katika nchi za Botswana,
Malawi, Namibia, Africa Kusini, Lesotho, Eswatini, Zambia, na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment