HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2019

CRDB yavuna faida Bil. 87 kwa miezi sita

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati akitangaza faida ya Sh. 87. Bilioni kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo, Frederick Nshekanabo. (Picha na Francis Dande).
Baadhi ya Wakurugenzi na Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa mkutanoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRD wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitangaza faida ya Sh. 87. Bilioni kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Joseph Witts na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo, Frederick Nshekanabo.


Na Mwandishi Wetu

BENKI CRDB, imetangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha Januari na Juni, mwaka  2019 ambayo ni ongezeko la asilimia 98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa ongezeko la faida hiyo limetokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara na jitihada binafsi za benki na ongezeko pato litokanalo na biashara za fedha za kigeni. 

“Mwaka 2019umekuwana mafanikio kwa Benki ya CRDB. Mapato na faida yetu vimeongezeka kutokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na mapato halisi yasiyo ya riba. Tulifanikiwa pia kuongeza kiwango cha mikopo huku tukishusha uwiano wa mikopo chechefu. 

Mikopo tuliyotoa kwa wateja iliongezeka sambamba na amana za wateja huku tukiwafikia wateja wapya kupitia huduma za kidijitali kama vile SimBanking, SIMAccount, mawakala wetu wa CRDB Wakala. Pia mapato yetu yameongezeka kufutia kuongezeka kwa pato litokanalo na ubadlishaji wa fedha za kigeni”  amesema Nsekela. 

“Tunajivunia ukweli kwamba tupo kwenye uelekeo mzuri kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea. Lengo si kuyafikia tu, bali Tunakusudia kuyavuka. 

Tutaongeza kasi zaidi ya utendaji hususani katika ubunifu na utoaji wa huduma za kidijiti zenye ubora wa juu. Tutaendelea  kuimarisha na kupitia mara kwa mara mifumo yetu ya utoaji huduma  kwa wateja ili kuhakikisha kuwa tunakidhi mahitaji ya soko.”

Katika kipindi cha Januari mpaka Juni 2019, mapato halisi ya riba ya Benki ya CRDB yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutoka TZS 198 bilioni ziilizokusanywa katika kipindi kama hiki mwaka 2018.

Aidha, rasilimali ziliongezeka kwa asilimia 8% kufikia shilingi 6.38 trilioni kulinganisha ni shilingi 5.93 zilizopatikana katika robo ya kwanza yamwaka 2019. 

Kwa upande wa amana za wateja wetu, ziliongezeka kwa asilimia 15% kufikia TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni zilizopatikana kwa robo ya kwanza yamwaka huu,” alisema Nsekela.

Nsekela alifafanua, Benki ya CRDB bado inaendelea kuwa na umiliki wa asilimia 22% ya thamani ya soko la mabenki hapa nchini hii kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wenye matawi 238, mashine za kutolea fedha 553 na Mawakala Zaidi ya 10,064 wa CRDB Wakala.

Kwa upande wa Amana za wateja, ziliongezeka kwa asilimia 15%  na kufika TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka.

Rasilimali za benki ilikua kwa asilimia 8% na kufika TZS 6.38 trilionikutoka TZS 5.93 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka.

Mapato ya riba yaliongezeka kwa asilimia 14% na TZS 315.4 bilioni kutokaTZS 276.8bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.

Mapato halisi ya riba yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutokaTZS 198bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.

Faida ghafi iliongezeka kwa asilimia 98% na kufikia TZS 86.6bilioni kutokaTZS 43.8bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.

Pia, faida halisi (baada ya kodi) ilikua kwa asilimia 108% na kufikiaTZS61.1 bilioni ikilinganishwa naTZS 29.3 bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

Pages