HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2019

Shirika la Posta lawataadharisha wateja wake

NA JANETH JOVIN

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) limewataarifu wateja wake na umma kwa ujumla kujihadhari na matapeli wanaotumia jina la Shirika hilo kwa nia ovu ya kuwaibia fedha kupitia ujumbe wa bahati nasibu hewa unaotumwa katika simu zao.

Shirika hilo limesema ujumbe huo wa bahati nasibu hewa unaotumwa na survey  kwa watu ili wajaze, walipie na wajishindie simu aina ya Apple iphone X na Samsung Galaxy S 10.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari ilijotolewa jana jijini Dar es Salaam na ofisi ya mahusiano ya shirika hilo ilieleza kuwa  matapeli hao wamefungua akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii na kutuma jumbe huo wa bahati nasibu hewa kwa wateja na wananchi.

"Shirika la Posta Tanzania(TPC) linatoa rai kwa umma kujiepusha na matapeli hawa. TPC haijihusishi kwa sasa na aina yoyote ya mchezo wa bahati nasibu ama survey ya aina yoyote inayowataka wateja na wananchi kuingiza nambari zao za account za benki ili kupata ushindi.

....Na jitihada za kuwasaka wahalifu hawa zinandelea ili wabainishwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria. TPC hutoa Taarifa zake sahihi zinazohusiana na huduma zetu
kupitia vyombo vya habari, kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Shirika  pamoja na tovuti rasmi ya Shirika," ilieleza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages