HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 31, 2019

GP SIRRO AKUTANA NA IGP WA SUDAN

 Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed Bashair, ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa nchi za Afrika Mashariki na Kati EAPCCO, wakati wa kikao Kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed Bashair ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa nchi za Afrika Mashariki na Kati EAPCCO, akizungumza jambo wakati wa kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro. Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudani yupo Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani, Adil Mohamed Ahmed Bashair ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati EAPCCO, akisaini kitabu cha wageni kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro. Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudani yupo Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
 

Na Mwandishi Wetu
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati EAPCCO katika mkutano Mkuu wa 21 wa umoja huo utakaofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 20 mwezi semptemba mwaka huu, Jijini Arusha katika ukumbi wa
AICC.

IGP Sirro amesema kuwa umoja huu ni msaada mkubwa wa kutatua changamoto za kihalifu zinazovuka mipaka ambazo ni wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu, Biashara ya haramu ya dawa za kulevya na uhalifu wa kimtandao kama changamoto ambazo nivigumu kwa nchi moja kukabiliana nazo kwa mafanikio
bila kushirikisha nchi nyingine. 

Aidha IGP Sirro ameusifu uongozi wa sasa wa umoja huu ambao Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudani, Adil Mohamed Ahmed Bashair kwa kufanikisha kutoa mafunzo kwa askari Polisi waliopo katika nchi wanachama sambamba na kuhakikisha kuwa nchi zote zinakuwa na utulivu.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na mwenyekiti wa umoja huu anayemaliza muda wake Mkuu wa Jeshi la Polisi la Sudani pamoja na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Polisi Makao Makuu ya Polisi Jijini Dar es
Salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudani amesema kuwa anaimani dhabiti na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Sirro na kwamba anaamini EAPCCO itakuwa katika mikono salama pindi atakapokabidhiwa uenyekiti wa umoja huo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Sudani yupo nchini Tanzania, Jijini Dar es Salaam kwa ziara siku mbili ya kikazi kuanzia tarehe 29 na 30 agosti mwaka huu. Shirikisho la Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki na kati -EAPCCO hadi sasa linaunaudwa na Burundi, Comoros, Djibouti, DRC, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, South Sudan, Sudan, Tanzania na Uganda. Nchi za mwisho kujiunga na umoja huo ni Burundi Democratic Republic of Congo ambazo zilijiunga tarehe 14 septemba 2017.

No comments:

Post a Comment

Pages