Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu michezo mkoani Kagera.
NA LYDIA LUGAKILA, BUKOBA
Serikali ya Tanzania imejipanga kumaliza changamoto
ya miundombinu mibovu ya viwanja vya mpira nchini ili kuiwezesha
sekta ya michezo kufanya vizuri.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa mkoani Kagera
katika mkutano na wadau wa sekta ya
habari utamaduni sanaa na michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo
Manispaa ya Bukoba .
Waziri Mwakyembe amesema kuwa
anatambua sekta ya michezo kuwa sehemu
muhimu na kuwa wana michezo wanafanya
kazi kubwa licha ya kukumbana na
changamoto ya miundo mbinu mibovu ya viwanja vya michezo.
amesema
kuwa tatizo hili la miundo mbinu mibovu ya viwanja limekuwa likipigiwa
kelele mara kwa mara na wanamichezo
licha ya kuonyesha juhudi kubwa katika
michezo kwa kuendana na miundo mbinu hiyo mibovu.
‘’ changamoto hii itamalizika mwaka
huu tutalifanyia kazi jambo hili ili
kupunguze kelele za viwanja vibovu vya soka nchini.
Katika hatua nyingine waziri Mwakyembe
amewataka wananchi mkoani Kagera
na Mikoa ya jirani kuwa septemba
4 mwaka huu.
Licha ya Changamoto hiyo waziri huyo
amewasihi wana michezo hao kutokata tamaa huku akiitaka Mikoa ya jirani na wana kagera kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi Septemba 4 mwezi hujao kuishangilia timu ya taifa stars inakutana kumenyana na timu ya Burundi mchezo ambao ameuataja kuwa ni muhimu sana kwa watanzania utakaifanya timu ya
taifa kufuzu kuingia kwenye kombe la dunia.
‘’ Siri kubwa
ya mafanikio ni mazoezi Vijana hakuna kusema kiatu kimebana tunakwenda
kuifunga Burundi ninachowaomba wana kagera wabunge wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania na mikoa jirani twendeni Burundi tukaishangilie timu yetu’ alisema.
Hata hivyo Amesema kuwa Rekodi ya
Tanzania ni nzuri kwani timu ya watoto wa kike chini ya miaka 17 ilikaribishwa
afrika kusini kimichezo na kuwabamiza
mabao 8-0 na kurudi Tanzania na kombe ikiwa ni mara ya tatu kuchukua ubingwa.
No comments:
Post a Comment