HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2019

Huduma vyeti vya kuzaliwa yatua Nane Nane-Simiyu

Afisa Usajili Msaidizi, Bw. Hidary Malick, kutoka Ofisi ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) akitoa maelekezo juu ya huduma za RITA kwa mteja.

Na Mwandishi Wetu, SIMIYU
WAKALA  wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA),unaendelea na zoezi la kusajili na kutoa cheti cha kuzaliwa kwa kila mwananchi asiyekuwa nacho Nyakabindi mkoani Simiyu.
                                
Zoezi hilo lililoanza hivi karibuni linafanyika katika viwanja vya maonesho  nanenane, ambapo wananchi mbalimbali wamekuwa wakijitokeza kupata huduma hizo.

Akiongea kutoka katika banda la RITA, Afisa Usajili Mwandamizi  Richard Ndeka alisema  kuwa wamejipanga vizuri kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wale wote ambao wamezaliwa Tanzania Bara lakini hawana cheti cha kuzaliwa hivyo tunawasihi wananchi hao  wajitokeze kwa wingi  ili kupata huduma hiyo.

"Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu inayotumika katika nyanja mbalimbali za mahitaji ya binadamu kama vile elimu, ajira,kupata mikopo ya elimu ya juu, Bima ya afya, pasi ya kusafiria pia,"

"Hatahivyo cheti hiki kinaonesha utambulisho wa kwanza wa mwananchi mwenyewe kwa maana ya mahali alipozaliwa, majina ya mtoto, majina ya wazazi,tarehe ya kuzaliwa pamoja na ubini wa muhusika,"alisema Ndeka.

Afisa Habari wa RITA,  Grace Kyasi alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa huduma nyingi zinazohitaji mtu awe na cheti cha kuzaliwa imepelekea asilimia kubwa ya wananchi kuona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na cheti hicho mapema.

"Cheti cha kuzaliwa kimekuwa kikitumika kupata huduma mbalimbali kama vile kupata elimu ya msingi,sekondari, kupata huduma ya afya,kupata ajira katika taasisi za Serikali, jeshini na sekta binafsi. Hata hivyo cheti cha kuzaliwa humpa mtoto haki za kurithi mali za wazazi wake. alieleza.

Alisema mtu yeyote aliyezaliwa katika ardhi ya Tanzania Bara bila kujali umri ,jinsia au mahali anapoishi anastahili kupata cheti cha kuzaliwa .

Alisema ili mtu aweze kupata cheti hicho  anapaswa kuwa na kiambatisho mbalimbali kati ya tangazo la kizazi kutoka kituo cha tiba alichozaliwa mtoto Kadi ya kliniki ya mtoto,Cheti cha ubatizo,Kadi ya kliniki ya mtoto, Kadi ya kupiga kura pamoja na kadi ya uraia.

RITA inashiriki katika maonesho ya nanenane kitaifa mkoani Simiyu yaliyoanza Agosti mosi  hivyo inawasisitiza wananchi waliokaribu na viwanja vya nanenane kutembelea katika banda lao lililopo karibu na bustani ya Suma JKT ili kufaidika na huduma mbalimbali za Wakala ikiwemo kupata cheti cha kuzaliwa. 

No comments:

Post a Comment

Pages