Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Uongozi
wa hotel ya Impala na Naura hatimaye umelipa mishahara ya miezi miwili
kwa wafanyakazi wake zaidi ya 257 waliokuwa wakidai na hivyo kuondoa
Malalamiko yaliyojitokeza.
Uongozi wa Impala umesikitishwa na taarifa zilizoandikwa kupitia mitandao
ya kijamii kuwa hotel hiyo imefilisika na kushindwa kujiendesha ikiwemo
kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na kudai kuwa jambo hilo si kweli
kwa kuwa limelenga kuwachafua kibiashara.
Mkurugenzi
wa hotel ya Impala na Naura ,Randy Mrema alisema wakati akiongea na
vyombo vya habari mapema Leo kuwa ,hotel zao bado zipo imara na
kuwataka Wateja kutokuwa na hofu juu ya changamoto ndogo za mishahara ya
wafanyakazi zilizojitokeza kwani jambo hilo ni mpito na limemalizika.
Alisema
hotel za Impala na Naura ni hotel za Kitalii zenye uwezo wa kuwahudumia
wageni wa aina mbalimbali duniani na wataendelea kushirikiana na
serikali katika kuhakikisha wanakuza sekta ya utalii nchini kupitia
hotel zao.
"Unajua
tumeshtushwa sana na taarifa ambazo zimekuwa zikienea kwenye mitandao
ya kijamii kwamba impala group imefilisika tunaomba wanaoeneza waje
kwetu kupata taarifa sahihi na si vinginevyo" alisema Mrema
Alisema
suala la wafanyakazi kutolipwa mishahara limekuwa likikuzwa na watu
wenye nia mbaya kibiashara ili hotel hizo zionekane kuwa hazifai jambo
ambalo si kweli.
Mkurugenzi
huyo amewaomba wafanyakazi wake kuendelea na mshikamano wao wa siku
zote tokea awali ili kuendeleza sekta ya Hotel za kitalii nchini na
kuondoa malalamiko yasiyokuwa na tija ambayo yanaharibu mahusiano mazuri
baina ya uongozi na wafanyakazi.
Alieleza
kuwa impala group inategemewa na wakulima zaidi ya mia tano wanaokuja
kuuza mazao yao ya mboga mboga na matunda wakiwemo pia wafugaji ambao
wamekuwa wakiiuzia kampuni yetu na kujipatia kipato hivyo haoni sababu
ya wao kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi hao.
Aidha
alisema kuwa baadhi ya watoa huduma za taxi na bodaboda waliopembeni
ya hotel hizo wamestushwa na kusikitishwa na taarifa za hotel hizo
kufilisika ambapo jambo hilo sio kweli na limeharibu taswira ya
kibiashara ya hotel hizo zilizo chini ya Impala group.
Alisema
kuwa kimsingi hakuna jambo kama hilo la kufilisika na kuwataka wale
wanaoharibu taswira nzuri ya impala group kuacha kufanya hivyo na tetesi
kama hizo sio nzuri kibiashara.
Awali
Mkurugenzi huyo pamoja na msaidizi wake Joram walidaiwa kuwekwa
mahabusu kwa saa 24 kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro
baada ya kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara yao jambo ambalo
wanasema walishawalipa mishahara yao.
No comments:
Post a Comment