Serikali imewaomba wananchi, hasa wa
maeneo mbalimbali nchini waanze ufugaji wa mazao ya zamani kutokana na
uhitaji mkubwa wa mazao hayo duniani.
Hayo
yamelezwa na Mtaalamu wa Mifugo na Uvuvi wizara wa mifugo na uvuvi
katika viwanja vya Themi, jijini Arusha akitoa ufafanuzi kwa wananchi
waliotembelea mabanda ya maonesho ya wakulima ( Nanenane) kanda ya
Kuskazini.
Alisema
serikali imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka nchi mbalimbali duniani ya
mazao ya uvuvi, hasa vyakula vinavyotokana na mazao ya bahari. Hata
hivyo kiwango cha uzalishaji ni kidogo kuliko mahitaji.
Alisema
mazao ya uvuvi yanasoko kubwa duniani kuliko biashara nyingine ambazo
baadhi ya watu wanalazimisha kufanya, japokuwa ni haramu na kosa kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Kwakuzingatia
ukweli huo,wananchi watakiwa kupata elimu ili wajikite katika ufugaji
waweze kujikwamua kiuchumi na wachangie pato la taifa kupitia sekta ya
uvuvi.
''Watu
wanalalamika umaskini lakini kuna fursa nyingi. Sisi tunaomsaidia
mheshimiwa Rais tunawajibu wakuwaonesha wananchi fursa hizo,'' alisema.
Mtaalamu
huyo wa wizara yenye dhamana ya uvuvi na mifugo alisisitiza kwamba
mkakati wa serikali ni kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda. Kwahiyo
ili kufikia azima hiyo malighafi zinahitajika.
Ulega
katika kudhihirisha wananchi watumie fursa hiyo alisema baada ya
kufanikiwa kutokomeza tatizo la uvuvi haramu kwa 90%, kwahiyo sasa
nimuda wa viongozi kusimamia utoaji elimu kwa wananchi kuhusu ufugaji.
Katika
kuhakikisha azima hiyo inatekelezwa kikamilifu amewaagiza maofisa na
wataalamu wa idara ya uvuvi waandae miradi. Kwani miongoni mwa sifa za
kiongozi na mtaalamu mzuri ni uwezo wa kubuni miradi na mambo yenye
tija.
Aidha Ulega
amewataka viongozi na watendaji ambao maeneo yao yanashughulisha na
uvuvi wahakikishe maeneo yao, hasa ya Pwani yanatumika kwa faida. Kwani
maeneo hayo hayatumika kikamilifu.
No comments:
Post a Comment