NA TIGANYA VINCENT
MATUMIZI ya shilingi
milioni zenye 20 utata katika mradi wa ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika
Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega umesababisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa Mzee Mkongea Ali akatee kuuzindua.
Hatua hiyo imefikiwa jana
wakati wa Mbio za Mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya
Nzega.
Alisema kwenye taarifa
yao waliyosoma imeonyesha kuwa wametumia milioni 540 kukamilisha ujenzi wa Wodi
hiyo lakini baada ya kupitia taarifa za malipo fedha na kuzijumulisha wamekuta
zimetumika milioni 560 ikiwa ni ongezeko la milioni 20.
Ali aliongeza kuwa utata
mwingine uliojitokeza ni ununuzi wa lita 300 za dawa ya kuua mchwa kwa gharama
ya milioni 10.
Alisema kiwango cha dawa
hicho ni kingi kulinganisha na eneo la ujenzi jambo ambalo linatia shaka na
kuacha maswali mengi.
Ali alimtaka Kiongozi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Nzega kupitia
nyaraka zote zinahusu mradi huo na ndani ya wiki watoe taarifa na kama kuna
ubadhirifu wahusika wachukuliwe hatua na kama matumizi yako sahihi Mkuu wa
Wilaya aweke jiwe la uzinduzi kwa niaba yake.
Aliwaonya watumishi wa
umma kuwa waadilifu wanaposimamia miradi ya umma ili kuhakikisha fedha
zilizotolewa linatumika kwa malengo yaliyopangwa.
No comments:
Post a Comment