NA TIGANYA VINCENT
JUMLA ya wakazi 552 wa
Halmashauri ya Nzega Mji wamejitokeza kupima virusi vya UKIMWI wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru katika eneo hilo.
Takwimu hizo zimetolewa
leo na Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi
wa Taifa Mbio za Mwenge wa uhuru Mzee Mkongea Ali.
Alisema katika zoezi hilo
wanaume wameongoza kwa kujitokeza kwa wingi ambapo 448 walipima na wanawake
walijitokeza ni 103.
Ngupula aliongeza kuwa
kati ya hao ni watu 8 ndio waligundulika kuwa na VVU ambao wanaume ni 6 na
wanawake ni 2.
Naye Kiongozi wa Mwenge
wa Uhuru Kitaifa Ali aliwataka wale wote ambao wamepima na kukutwa na VVU
kuzingatia ushauri waliopata na kuanza matumizi ya dawa za kufumbaza VVU.
Alisema kwa wale ambao
wamekutwa hawana VVU kuwa waaminifu katika ndoa zao
No comments:
Post a Comment