HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 07, 2019

WANAFUNZI WA LINDI SEKONDARI WAASWA KUSOMA KWA BIDII

 Mkuu wa Kitengo cha Udahili Kurugenzi ya Shahada za Awali Chuo kutoka Kikuu cha Dar es Salaam  Victoria Lyimo  akiwapa maelezo  wanafunzi wa Lindi Sekondari wakati wa Ziara fupi iliyofanywa shuleni hapo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Dk. Arnold Towo  akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wakati wa ziara fupi katika Shule ya Lindi Sekondari.
 
Lindi, Tanzania
 
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kimetembelea na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Mkoa wa Lindi.

Akizungumza na wanafunzi hao, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Dk. Arnold Towo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwataka wawe wabunifu na wenye kujituma katika masoma yao.

Jambo la msingi sana kwenu ni kujitambua na kuchagua masomo yale ambayo yatawasaidia katika maisha yenu ya baadae.

“Nawaomba sana mjitume na kutumia nafasi mnazopata ikiwa ni pamoja kufanya midahalo itakayowasaidia kuwajengea uwezo wa kujieleza, hii itawasaidia pale mtakapomaliza masomo na kujiandaa na ajira”, alisisitiza Dk. Towo.

Aidha Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Kurugenzi ya Shahada za Awali, Victoria Lyimo, aliwasisitiza wanafunzi hao kuwa Wachamungu, kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii kwa kuzingatia haya hata kwenye Masomo yenu mtaweza kufanya vizuri sana.

Shule ya Lindi Sekondari kidato cha Tano na Sita inamichepuo ya HKL, HGL, EGM, PGM na HGK katika masomo haya wanafunzi wameaswa kusoma kwa bidii ili waweze kuwa na ufaulu mkubwa utakao wasaidia pindi wanapotaka kujiunga na Chuo Kikuu.

Hii ni sehemu mojawapo ya jukumu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Huduma kwa Umma kurudi kwa jamii kuzungumza na kutoa hamasa kwa wanafunzi mbalimbali nchini katika Masuala ya Elimu,Tafiti na Ushauri.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kupitia ndaki  ya Sayansi ya Kilimo na Ufugaji wa Samaki wa Kisasa kimeshiriki katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane yenye kauli mbiu isemayo “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi” kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2019 katika Viwanjanvya Ngongo Kanda ya Kusini Mkoani Lindi ambapo kilele cha maonesho hayo ni kesho Tarehe 8 Agosti, 2019.

Imetolewa na Afisa Uhusiano Idara ya Huduma kwa Umma.

No comments:

Post a Comment

Pages