HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 08, 2019

MABONDIA WATAKAOBUKA NA USHINDI AGOSTI 24 KUPEWA BIMA YA AFYA YA MWAKA MMOJA BURE

SELEMANI SEMUNYU
 
Homa ya Mapambano ya Ubingwa Afrika Mashariki na kati imezidi kupanda baada ya kampuni ya bima ya Resolution kutoa bima ya Afya ya mwaka mzima kwa mabondia watakaoibuka na ushindi wa mikanda hiyo.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Resolution Insurance Maryanne Mugo alisema mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo ambayo wachezaji wake wana kila sababu kuwa na bima ya afya.

"Huu ni Mwanzo lakini nina amini Mabondia wengi watahamasika na kujiunga na Bima ya Matibabu ili waweze kupata matibabu pale inapohitajika.

Kwa upande wake Mratibu wa kiufundi wa pambano hilo Yassin Abdalah amesema ujio wa resolution na kuboresha zawadi kwa washindi ni jambo la kupongezwa kwani uwepo wa wadhamini katika ngumi ni jambo muhimu kwa maendeleo ya mchezo huo.

Aliongeza kuwa katika Masuala yote ya Kiufundi yanaenda vizuri ikiwemo afya za mabondia na wanaendelea na mazoezi kwama walivyopangiwa na walimu wao.

Aliwataja Mabondia hao kuwa ni Nasibu Ramadhani na Issa Nampepeche wakati Haidary Mchanjo na Tonny Rashidi na katika Mapambano ya Utangulizi Lukmani Ramadhani vs Ismail Haridi Bakari Dunda na Kudura Tamimu.

Naye Mratibu Mkuu wa Pambano hilo Selemani Semunyu alisema licha ya kuwepo kwa mapambano hayo pia kutakuwa na Mapambano ya  Mabondia kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaojiandaa na Mashindano ya Dunia ya Majeshi Nchini China.

Semunyu alisema Mabondia hao wataongozwa na Koplo Selemani Kidunda lengo likiwa ni kujipima kuelekea Mashindano hao na kutia hamasa kwa Wananchi na Mabondia

Pambano hilo la Ngumi linalotarajiwa kufanyika Agosti 24 Mwezi huu limeandaliwa na Club 361 kwa kushirikiana na PeakTime na Solid Rock na kudhaminiwa na Smart Gin, Kiwango Security na Resolution Insurance.

No comments:

Post a Comment

Pages