Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) alipotembelea leo. Kushoto ni Dkt. Juma Mfinanga akiwa na Waziri Ummy
Mwalimu baada ya kumweleza jinsi MNH ilivyojiandaa kuwahudumia wajumbe wa
mkutano wa SADC pamoja na wananchi wengine.
Daktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. William Mugisha (kulia), akimweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kuhusu huduma ya upasuaji wa mivunjiko ya kikombe cha mfupa wa nyonga alipotembelea banda la MOI.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo akimweleza Waziri Ummy Mwalimu huduma zinazopatika JKCI zikiwamo huduma za tiba ya umeme wa moyo na kuzibua mishipa ya damu.
Daktari wa Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, Dkt. Andrew Laiser akieleza jinsi walivyojiandaa kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC na wananchi wengine.
Waziri Ummy Mwalimu akisoma jarida la Muhimbili linaloeleza huduma mbalimbali za afya zinazopatikana MNH. Kulia ni Dkt. Juma Mfinanga akimweleza jambo Waziri.

Afya Ummy Mwalimu, wataalam wa afya pamoja na wataalam wengine wakiwa katika viwanja
vya ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kukagua mabanda na
kliniki zitakazotumika kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC.
Wataalam wa
afya wa Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Lugalo wakiwa katika picha ya
pamoja na Waziri Ummy Mwalimu leo katika viwanja vya ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). (Picha na John Stephen).
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amezikaribisha nchi wanachama wa SADC kutumia
huduma za ubingwa wa juu zinazopatika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi
ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Mhe. Ummy
ameyasema hayo leo alipotembelea mabanda
ya MNH, MOI na JKCI yanayoshiriki maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja
vya ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNICC) kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya
nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza mapema wiki hii.
Waziri Ummy
amesema Wizara yake imeweka wataalam wa afya ili kutoa huduma kwa wajumbe wa
mkutano wa SADC watakaohitaji huduma za matibabu pamoja na wananchi wengine
watakaokuwapo katika viwanja hivyo.
Aidha
ameziomba nchi za SADC kupata huduma za ubingwa wa juu zinazopatikana MNH kama upandikizaji figo
(kidney transplant), upandikizaji watoto vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear
implant), tiba kwa njia ya radiolojia (interventional radiology).
Kwa upande wa MOI, Waziri
Ummy amezitaka nchi za SADC kuja kupata huduma za upasuaji wa mivunjiko ya
kikombe cha mfupa wa nyonga, upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia na
upasuaji wa magoti, ubongo na mgongo kupitia matundu madogo.
Kwa upande
wa JKCI amezitaka nchi za SADC kupata huduma za tiba ya umeme wa moyo, kuzibua
mishipa ya damu na upasuaji wa kufungua kifua kwa ajili ya kurekebisha valvu au
matundu kwenye moyo.
“Kama Wizara tumeweka wataalam wa afya hapa
eneo la mkutano ili kutoa huduma kwa
wajumbe wa nchi za SADC. Wataalam wetu wa Muhimbili, MOI, JKCI na pamoja Hospitali ya Lugalo wako tayari kuhudumia
wageni wetu ambao watapata changamoto yoyote ya kiafya,” amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy ametembelea
kliniki maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wageni na wananchi
mbalimbali wanaotembelea maonesho ya viwanda na maandalizi ya mkutano wa 39 wa
SADC.
No comments:
Post a Comment