Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii imetoa pikipiki
kwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ili waweze kuwafikia wanawake wa wa mjini na
vijijini kwa lengo la kuwahamasisha ili waweze kumiliki na kushiriki kukuza
uchumi hapa Nchini.
Akiongea leo Jijini Dodoma Mkurugenzi Idara ya Jinsia Bw.
Juluius Mbilinyi kutoka Wizara aya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii amesema
kuwa wataalam hao wanapatiwa vifaa hivyo vya usafiri ili wawaeze kutoa elimu na
kuhamasisha wanawake kuweza kumiliki na kushiriki zaidi katika uchumi wa
viwanda.
Aidha Bw. Mbilinyi ameongeza kuwa Wizara imejipanga kuwapatia
wanawake kote Nchini fursa za kiuchumi kwa kuwapatia fursa za masoko lakini pia
kuhakikisha wanatumia teknolojia raisi itakayowawezesha kuzalisha mali kwa
wingi zaidi bila kutumia ghalama kubwa kuwekeza katika teknolojia ya juu.
Bw. Mbilinyi amezitaja takwimu za uchumi wa kaya kuwa
zinaonesha kaya zinazoongozwa na wanawake bado umasikini uko kwa 27% wakati
zile za wanaume kiwango cha umasikini ni 26% akiongeza kuwa wastani wa kiwango
cha umasikini kwa kaya ni 24%
akisisitiza kuwa ndio maana nchi inajikita katika kuwezesha wanawake kiuchumi.
Bw. Mbilinyi ameutaja Mpango wa Taifa wa miaka mitano wa
kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kuwa unasisitiza kuwa
hatuwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa kuwaacha wanawake Nyuma ndio maana
serikali kupitia Wizara ya Afya imejikita sana katika kuwainua wanawake kiuchumi.
Wakati huohuo Mkurugenzi msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Mboni
Mgaza ameongeza kuwa Wizara imetoa pikipiki 25 kwa Mkoa wa Dodoma ili
kuhakikisha Wanawake wajasiliamali wanafikika popote walipo akitaja pikipiki
hizo kuwa nyenzo muhimu ya kuwawezesha
Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoa huduma kwa wanawake hao.
Bi. Mboni amesema kuwa
baada ya Wizara kuona kuwa ni vigumu kuwafikia wanawake wengi bila
usafiri iliamua kwa nia moja kutafuta namna ya kuwaezesha wataalam ili waweze
kufika katika vikundi vya wanawake hao ili kuwahamasisha na kuwapatia elimu ya
maendele uku akiongeza kuwa zoezi kama leo litaendelea mapema mwezi huu katika
Mkoa wa Katavi ambnapo Wizara yake itakabidhi pikipiki 15 kwa Maafisa Maendeleo
Mkoani humo.
Mapema wiki iyopita Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan alizindua zoezi la ugawaji pikipiki kwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii
Mkoani Dodoma zoezi lililowashirikisha viongozi wa Wizara, Mkoa pamoja na
Maafisa Maendeleo wa Mkoa na Wilaya za Dodoma.
No comments:
Post a Comment