HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2019

VIGOGO UPINZANI WAJIUNGA NA CCM

Na Lydia Lugakila, Kagera

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Kagera, Ilidephonce Murokozi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bubale Kata ya Kakunyu, Joseph Azine, kupitia Chadema wamepokea kadi na kiapo cha kujiunga na CCM ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli.

Akiongoza kiapo hicho Septemba 13 mwaka huu katika viwanja vya chama cha Mapinduzi CCM vilivyopo katika kata ya Kakunyu katibu wa chama cha mapinduzi CCM Halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Hassani Moshi amewataka viongozi hao wapya kufuata miongozo ,sheria,na Kanuni za chama hicho ili kulinda na kukiimalisha chama .

Moshi amesema viongozi hao waliorejea katika chama hicho hawana budi kuendana na kasi ya Rais Magufuli katika kuhakikisha taifa na wananchi wawatumikiao wanakuwa na maendeleo Endelevu.

Katibu huyo amesema wanachama hao wapya waliorejea na kupokelewa rasmi leo walirejesha kadi za vyama vya mnamo Agost 8, 2019 na kuwataka wananchi na viongozi wa chama hicho kuwapokea kwa mikono miwili na kuwapa haki sawa na Mwanachama aliyeishi miaka 30 ndani ya chama hicho.

Kwa upande wake katibu mwenezi CCM wilaya ya misenyi Kamuzora Coronery amewapongeza wanachama hao wapya na kuwahimiza kuwatumikia wananchi wao vyema lli kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Joseph William na Ilidephonce Vedasto Murokozi ambao ni warejea wapya wa chama cha Mapinduzi CCM wameaahidi viongozi hao wa wilaya kuhakikisha wanafuata miongozo, sheraia ,kanuni za chama hicho kwa asilimia mia moja.

Katika shughuli hiyo katibu wa chama cha mapinduzi CCM Halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Hassani Moshi amewapokea makada wa kike 3 na kuwapatia kadi za chama hicho huku akisisitiza wakina mama kujitokeza katika Kugombea nafasi mbali mbali za chama na kuacha dhana ya kuwa wanaume ndio wanaouwezo wa kuongoza peke yao.

No comments:

Post a Comment

Pages