HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2019

WANAWAKE WATAKIWA KUACHA UOGA KATIKA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Katibu CCM Wilaya Misenyi, Hassani Moshi, akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi wawili waliotka upinzani.
 

Na Lydia Lugakila, Kagera


Katibu wa CCM Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Hassani Moshi ametoa agizo kwa Makatibu Kata wilayani humo kufunga madaftari yote ya wanachama kwa ngazi ya matawi ya kata ifikapo Septemba 17, 2019.


Agizo hilo limetolewa Septemba 13, 2019, wakati akiwa katika Kata ya Kakunyu wilayani Misenyi katika akiwapokea na kuwaapisha aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Kagera, Ilidephonce Murokozi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bubale katika kata hiyo Joseph Azine, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliorejea na kuvihama vyama vyao kujiunga na CCM.


Mhe. Moshi akitoa maelekezo hayo na kuwataka Makatibu Kata wilayani Misenyi hiyo mkoani hapa kuhakikisha wanafunga Madaftari yote ya wanachama kwa ngazi ya matawi ya kata ifikapo Septemba 17 mwaka huu.


Amesema kwa yeyote atakayekiuka utaratibu huo atakuwa anajitafutia sababu ikiwemo kukaa kwa vikao vitumie kanuni na katiba ‘’Natoa Agizo hili kwa atakayekiuka sio mimi nitakayeamua ni Katiba’’ amesema

Hata hivyo amewataka wananchi hasa wanachama wa CCM wilayani humo kujitokeza kwa wingi hasa wakina mama na kuwataka kutowaogopa wanaume kwenda kugombea nafasi za wenyeviti na kuwa wasisubiri nafasi za viti maalum.

No comments:

Post a Comment

Pages