HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2019

Bil.93.8/- zatumika kuboresha miundombinu ya elimu

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, akiwasili kwenye Mkutano wa Viongozi wa Wizara hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
 Meza Kuu.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, akifungua Mkutano wa Viongozi wa Wizara hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza kwenye Mkutano wa Viongozi wa Wizara na Wahariri wa vyombo vya habari.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Dk. Adolf Rutayuga, akizungumza katika mkutano huo.
 Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wahariri.
 Mkuu wa Idara ya Mawasiliano kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoljia, Sylvia Lupembe, akizungumza katika mkutano huo.
Kamishna wa Elimu wa Wizara hiyo, Dk. Lyabwene Mtahabwa, akitoa mada kuhusu mafanikio katika uboreshaji wa Elimu Msingi, Maalumu na Ualimu.  
Baadhi ya Wahariri walioshiriki mkutano huo.
 


NA IRENE MARK
 
SERIKALI imetumia Sh. bilioni 93.8 kuimarisha miundombinu kwenye shule 588 za msingi na sekondari zikiwemo shule kongwe.

Akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Leonard Akwilapo, alisema kazi kubwa imefanyika kuboresha elimu hapa nchini.

Dk. Akwilapo alisema kiwango cha elimu kimeongezeka huku ubora wa ufaulu wa wahitimu wa ngazi mbalimbali ukiendelea kustawi.

Alisema pia wizara inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 ili kufanyia maboresha yatakayokwenda na wakati.

Aliwataka pia viongozi wa sekta ya elimu kushirikiana na waandishi wa habari ili kuhakikisha jamii inapata habari sahihi kwa wakati.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora katika wizara hiyo, Valeria Mushi, alisema mwaka 2019/2020 serikali itajenga ofisi 55 za udhibiti ubora kwenye halmashauri 55 na kwamba mwaka uliopita tulijenga ofisi 100 kwenye halmashauri mbalimbali.

“Asilimia 80 ya ofisi hizo zimekamilika na nyingine zipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika kwake… kwa hiyo kwa miaka hii miwili tutakuwa na ofisi 155 za udhibiti ubora wa elimu, lengo ni kuboresha utendaji kazi na elimu.

“…Wadhibiti ubora wengi walikuwa hawana ofisi mazingira yalikuwa sio rafiki lakini sasa watafanyakazi kwenye mazingira bora hivyo kuisimamia elimu kwa viwango vya juu. Lengo ni kuzifikia halmashauri zote 184 zipo hapa nchini.

Kuhusu rasilimali watu Mushi alisema jumla ya wadhibiti ubora wa shule za msingi na sekondari ni 1,595 huku akibainisha kwamba wapo wengine wapya 300 watakaoanza kazi baada ya kupewa mafunzo ifikapo Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages