HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2019

BRITAM YAIBUKA MSHINDI KAMPENI UELEWA 2019

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Ziwa, Jarlath Mushashu (kushoto), akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuregenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Britam, Raymond Komanga, kilichotolewa na Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) baada ya kuibuka washindi wa Kampeni ya Uelewa 2019 kuhusu masuala ya bima. (Na Mpiga Picha Wetu). 
NA SULEIMAN MSUYA

KAMPUNI ya Bima ya Britam imefanikiwa kuandika historia mpya baada ya kuibuka mshindi wa tuzo za Kampeni ya Uelewa mwaka 2019.

Britam imeibuka mshindi kupitia kampeni yake ambayo ilitambulika kwa jina la ‘Tupo na Wewe’ ambayo inatajwa kugusa jamii kubwa ya Kitanzania.

Akizungumzia ushindi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Britam, Raymond Komanga alisema zawadi hiyo imesaidia kuwaongezea nguvu kubwa katika kutoa huduma na mwelekeo wa wawao kutoa huduma za kimataifa zitakazokidhi hitaji la wateja wao.

Alisema zawadi hiyo imegusia vipengele saba ambavyo ni kampeni ya bima, ubunifu wa bidhaa za bima, ushirikiano na jamii, uibuaji wa wajasiriamali, tafiti, maendeleo na mawazo.

Mkurugenzi huyo alisema kampeni ya ‘Tupo na Wewe’ ina maana kila hatua ambayo wanapiga wanakuwa na wateja wao katika kuwapatia huduma hivyo kusaidia kubadilisha mtazamo kwa urahisi.

“Tumerfarijika sana kupokea zawadi hiyo ya heshima ambayo kwetu ni mafanikio makubwa. Ni matumaini yetu zawadi hii inatupa nguvu kufanya mambo mazuri na makubwa kwa wateja wetu,” alisema.

Komanga alisema zawadi hiyo imeonesha kutambua mchango wa sekta ya bima nchini pamoja na kututaka kuwa wavumbuzi na wabunifu katika sekta hiyo.

Alisema katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa Britam itaendelea kubuni na kuja na kampeni mpya ambazo zinaweza kusaidia jamii kupata uelewa kuhusu bima.

“Britam inasisitiza kuwa itaendelea kujitangaza na kutoa elimu ili kusaidia TIRA kufikia lengo lake la kutoa elimu ya bima kwa asilimia 45 ya Watanzania ifikapo 2021,” alisema.

Alisema Britam imekuwa ikitoa huduma za bima katika nchi saba za Afrika Mashariki na Kusini Tanzania ikiwemo hivyo wanaendelea vizuri kutoa huduma nzuri. Mkurugenzi huyo alisema Kampuni ya Britam hadi sasa ina matawi saba nchini ambayo yapo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Mtwara na wanatarajia kufungua tawi jipya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages