Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (katikati) wakisoma ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini katika eneo la Mitengo, Mtwara. Kushoto ni Meneja wa Mradi, Godwin Maro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima korosho nchini wahakikishe wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa wadau na wanunuzi.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote inayolima korosho nchini wahakikishe wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa wadau na wanunuzi.
“Mabadiliko ya
mifumo yalitolewa na baadhi ya viongozi ambao sio waaminifu, Serikali
iko macho itawachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa
waaminifu. Tunataka mfumo wenye manufaa ndio utumike.”
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Oktoba 2, 2019) wakati akizungumza na wananchi wa
mkoa wa Mtwara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya
Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo, wilayani Mtwara.
Waziri
Mkuu amesema msimu wa korosho kwa mwaka huu unatarajiwa kutangazwa hivi
karibuni, hivyo ni lazima kwa wakuu wa mikoa inayolima korosho
wakajiandaa vizuri ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.
Waziri
Mkuu ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi
wa korosho kwa njia ya kangomba.”Kangomba imepigwa marufuku,
watakaojihusisha moto utawawakia huko huko . Tunataka wakulima wenyewe
ndio wanufaike”
Pia,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakulima wa zao la korosho kuendelea
kujiimarisha na wahakikishe wanajiwekea akiba kwa ajili ya ununuzi wa
pembejeo kwa sababu. “Serikali itaendelea kusimamia zao hili ili
wakulima wapate tija.”
Mapema,
Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini
na kukagua kazi ujenzi inayoendelea hospitalini hapo, ambapo amesema
itakapomalizika itawapunguzia wananchi safari ya kwenda Muhimbili
kufuata huduma.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
imejikita katika kuboresha huduma mbalimbali za wananchi zikiwemo za
afya, hivyo wananchi wa Kanda ya Kusini watapata matibabu ya kibingwa
karibu na maeneo yao.
“Hakuna
mashaka wala wasiwasi wa kupata huduma bora za afya kuanzia sasa na
kuendelea kwa sababu Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwezesha utaratibu mzuri wa
kupata huduma za afya nchini.”
Ujenzi
wa hospitali hiyo ya Rufaa ya Kanda ya Kusini unatarajiwa kukamilika
Agosti 2020 na kwa sasa inajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 15 na tayari Serikali imeshatoa
zaidi y ash. bilioni sita.
Kwa upande wake, Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. Bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali hiyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
za afya
Alisema historia ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa Mkoani Mtwara ilianzia kwenye kikao cha Halmashauri
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi cha Mkoa cha tarehe 16 Januari 1979.
Halmashauri Kuu ilijadili na kuazimia kuishawishi Serikali kujenga
hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia Mikoa ya Mtwara,
Lindi na Ruvuma.
Waziri
Ummy aliongeza kuwa hospitali hiyo inajengwa kwa awamu, ambapo awamu ya
kwanza ilianza mwaka wa fedha 2005/2006 kwa kazi ya upimaji wa mipaka
na mwinuko wa ardhi kupitia kampuni ya Beacon Consult Ltd kwa gharama ya sh. 26,000,000 na ilikamilika ndani ya siku 30 za mkataba. Kwa sasa ujenzi huo upo katika awamu ya nne.
Awali,Waziri
Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo
katika eneo la Msijute mkoani Mtwara na kukagua kazi ya ubanguaji pamoja
na kuzungumza na watumishi wa kiwanda hicho ambao waliishukuru Serikali
kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment