HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 13, 2019

Kampuni ya Mars Communication yatoa msaada kwa Yatima

Ofisa Masoko wa Kampuni ya Mars Communication ambao ni mawakala wa bidhaa za Hisense, Wallu Amani (kulia), akikata keki na watoto wanaoishi katika Kituo cha Kulea Watoto wenye mahitaji Maalum cha Hisani Mbagala wakati wa hafla ya kutimiza miaka 50 ya bidhaa hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Na Mpiga Mpicha Wetu).
  
 
Na Janeth Jovin

KAMPUNI ya Mars Communication imetoa msaada wa  vyakula, nguo, sabuni na vinywaji  kwenye  vituo vya watoto yatima kilichopo Mbagala maji Matitu na Mwasonga Kigamboni jijini Dar es Salaam,  kwa lengo la kuwafariji na kurudisha shukrani kwa wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo jijini Dar es Salaam jana katika vituo hivyo,  Ofisa masoko wa kampuni ya hiyo Wallu Amani, anasema wanaadhimisha miaka 50 ya uwepo wa bidhaa yao Hesense Sokoni hivyo wameamua kurudisha shukrani kwa jamii kwa kutoa msaada huo.

Anasema wakati wanafurahia kutumiza miaka hiyo 50 wanatambua kuwa wapo watu wenye mahitaji maalum wanatakiwa kupewa msaada.

“Wakati tunatimiza miaka hii 50 sokoni, kuna watu wanauhitaji mkubwa walau wapate mlo wa siku lakini wanaukosa kutokana na changamoto za kimaisha, hivyo tumeamua kujumuika nao kugawana kidogo tulichonacho, ”anasema Amani na kuongeza

“Tumeamua kufanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii faida tuliyoipata ikiwapo na hivi tunavyokula kunya pamoja na watoto hawa ambao wengi wao hawana wazazi wala walezi hivyo ni jukumu letu kama wazazi pia kuhakikisha na wao wanafurahi kama watoto wengine” alisema Amani.

Hata hivyo hakuwa tayari kutaja thamani ya vitu walivyotoa kwa sababu ni sadaka na kusema  kugawana kinachopatikana ni utaratibu waliojiweka ambapo hufanya hivyo kwa kuwakopesha wafanyakazi wao pia.

Naye Mkurugenzi na mlezi wa kituo cha yatima cha Mbagala Hidaya Mutalemwa anasema kuwa anaishukuru kampuni hiyo kwa msaada waliowapatia na kuwaomba kampuni zingine kuiga mfano kama huo.

“Changamoto za kuishi au kulea watoto wenye mahitaji maalumu ni nyingi na ngumu, wakijitokeza watu kama Hesense inakuwa ni faraja.

“Jambo muhimu kwa watoto ni chakula na bima ya afya, hivyo tunawaomba wadau mbalimbali ikiwamo kampuni zinayotoa bima za afya watuangalie na ikiwezekana tupewe msaada wa kutibiwa bure au kwa gharama nafuu, ”anasema Hidaya.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho, Baraka Miraji (10)anasema yupo yeye na mdogo wake baada ya mama yao kuwatelekeza katika kituo cha daladala cha Mbagala Rangi Tatu  miaka mitano iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Pages