Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Erick Mapunda kuyavunja Mabaraza yote ya Kata na
Vijiji ya ardhi yasiyotenda haki wakati wa kutoa maamuzi katika wilaya ya Mafia
mkoani Pwani.
Dkt Mabula alitoa agizo
hilo tarehe 01 Oktoba 2019 akisikiliza kero za migogoro ya ardhi za wananchi wa
Baleni na Kilindoni wakati wa ziara yake ya siku mbili wilayani Mafia mkoani
Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi,
kukagua masijala ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi
kwa njia ya kielektroniki.
Alisema, kutokana na
kero nyingi za ardhi alizozipokea katika ziara yake hiyo wilayani Mafia
amebaini Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya hiyo hayafanyi kazi zake vizuri
na wajumbe wake wamekuwa wakiyatumia kutoa maamuzi yasiyozingatia haki.
Kwa mujibu wa Dkt
Mabula, kadri Mabaraza ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia yanavyofanya
vibaya katika utoaji maamuzi yake basi hata uanzishwaji Baraza la Ardhi la Nyumba
la wilaya hiyo halitafanya vizuri katika utendaji wake.
Cue
in ……………………………………NAIBU WAZIRI
Cue
out …………………………………. NAIBU WAZIRI
Kwa upande wake Mbunge
wa jimbo la Mafia Mbaraka Dau alielezea furaha yake ya kutaka kuanzishwa Baraza
la Ardhi la Nyumba la Wilaya ya Mafia ambapo alisema litasaidia kutoa haki kwa
wananchi wa mafia ambao baadhi yao wamekuwa hawapati haki kutokana na kushindwa
kwenda katika baraza la wilaya la Mkuranga.
Cue
in ……………………………..MBARAKA DAU
Cue
out……………………………MBARAKA DAU
Baadhi ya wananchi wa
Mafia wamelalamikia Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji katika wilaya ya Mafia pamoja
na kero nyingine mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa
zinachangia uwepo migogoro ya ardhi.
Mohamed Shaban na Aisha
Mohamed ni miongoni mwa wananchi wa Mafia waliowasilisha kero zao kwa Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na hapa wanazungumza:
Cue
in ……………………………..MOHAMED SHABAN
Cue
out………………………….....MOHAMED SHABAN
Cue
in ………………………………..AISHA MOHAMED
Cue
out …………………………….AISHA MOHAMED
No comments:
Post a Comment