HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 08, 2019

MILIONI 921,000,000 KUTATUA TATIZO LA BARABARA MKUTA - MPANGATAZARA

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani watatengeneza barabara hiyo ili ichochee maendeleo kwa wananchi.
 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani daraja hilo lipo hatarini kubomoka.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikagua moja ya madaraja ambavyo yamelalamikiwa kwa ubovu.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

JUMLA ya milioni mia tisa ishirini na moja zinatumika katika kutatua Tatizo la barabara kuanzia Mkuta hadi Mpangatazara kwa kiwango cha changalawe katika jimbo la Mufindi Kaskazini kwa lengo la kurahisisha shughuli za kimaendeleo ambazo zimekuwa zikihusisha barabara hiyo.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara ya mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi alisema kuwa pesa tayari imepatika na tayari wameshawapata wakandarasi ambao watatengeneza barabara hizo.

“Mheshimiwa mbunge na wananchi wako mwezi huu wa kumi tunaanza kutengeneza barabara hii ambayo imekuwa kimbilio la maendeleo kwa wananchi wa jimbo hili hasa katika biashara ya usafirishaji wa zao la mbao ambalo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini” alisema Mjohi

Mhandisi Mjohi alisema kuwa barabara hiyo inayotengenezwa itapita katika vijiji vya Ifwaji,Ifupira,Kidete,Ikanga,Ihanu,Ibwanzi,Lulanda,Isipii na Mpanga Tazara kwasababu vijiji hivi vipo barabarani kabisa lakini vijiji zaidi ya arobain vitanufaika na barabara hiyo kimaendeleo.

“Barabara hii ikikamilika itahudumia zaidi ya vijiji arobaini ambavyo vipo pembezoni au vinazungukwa kwa namna moja au nyingine na barabara hii ambayo imegharimu mamilioni ya pesa ambazo zimetafutwa na mbunge wa jimbo hili” alisema Mjohi

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa aliwahakikishia wananchi kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kuwa fedha ametafuta na amewakabidhi kwa TARURA wilaya ya Mufindi na tayari wameshapata wakandarasi wawili ambao watatengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe.

“Mimi mbunge wanu nimeshafanya kazi yangu ya kutafuta fedha nimepata na nimekabidhi kwa wataalam hivyo kazi iliyobakia ni kuhakikisha wataalum wanasimamia vilivyo barabara hii ili ijengwe kulinga na gharama ambazo zimetolewa” alisema Mgimwa

 Mgimwa mgimwa alisema kuwa barabara hiyo inaumhimu mkubwa kwenye biashara ya zao la mbao kwa kuwa ndio baishara kuu inayofanyika katika barabara hiyo na kuwakumbusha wananchi kuwa barabara hiyo ni yao na wanapaswa kuisimamia.

Nao wananchi waliendelea kumkubusha mbunge umuhimu wa barabara hiyo kimaendeleo kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiitumia katika shughuli za kimaendeleo za kila siku.

No comments:

Post a Comment

Pages