Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, akiruhusu msafara wa waendesha baiskeli Msata wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana, ambao utapita katika mikoa saba hadi Butiama mkoani Mara wakienzi kwa vitendo juhudi za Baba wa Taifa. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KUELEKEA kumbukumbu ya miaka 20 ya hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere tangu kifo chake, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete
amezindua msafara wa waendesha baiskeli.
Uzinduzi huo ulifanyika Msata wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
jana, ambapo waendesha baiskeli hao wanaelekea Butiama kupitia mikoa saba kwa
muda wa siku nane wakienzi kwa vitendo juhudi za Baba wa Taifa.
Katika uzinduzi huo, Kikwete amewataka viongozi wa waendesha
baiskeli nchini kupanga mipango mikakati ambayo itawasaidia kuendeleza na
kukuza mchezo huo kimataifa badala ya kutumia muda wa kuongelea changamoto.
Sanjari na hayo, Dk. Jakaya pia alipanda mti mmoja na
kumkabidhi kiongozi wa msafara Gabriel Mlanda mti mmoja ambao utapandwa
nyumbani kwa baba wa Taifa, Butiama mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment