Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akibonyeza kitufe kuzindua uunganishaji wa mtandao wa intaneti kwenye kompyuta zilizotolewa na UCSAF na Vodacom kwenye shule za sekondari za mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, Roselyn Mworia akimwonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) kompyuta
iliyounganishwa na intaneti kwa ajili ya wanafunzi kujifunza na waalimu kufundishia akiwa shule ya sekondari ya Simiyu mkoani Simiyu.
iliyounganishwa na intaneti kwa ajili ya wanafunzi kujifunza na waalimu kufundishia akiwa shule ya sekondari ya Simiyu mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akimkabidhi mwalimu wa shule ya sekondari Itilima, Flora Shimbi kompyuta mpakato na kifaa maalumu kwa ajili ya kuunganisha shule za sekondari za mkoa wa Simiyu kwenye mtandao wa intaneti. Tukio hilo limefanyika sekondari ya Simiyu mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa huo kabla ya uzinduzi wa uunganishaji wa shule kwenye mtandao wa intaneti na kompyuta walizopewa na UCSAF na Vodacom. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Na Prisca Ulomi, Simiyu
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amezindua uunganishaji wa shule za sekondari za Mkoa wa Simiyu kwenye mtandao wa intaneti kwa kuzifunga kompyuta mia moja zilizotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kompyuta za mpakato ishirini zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kwenye mtandao wa intaneti ili wanafunzi waweze kutumia huduma ya mtandao kujifunza na waalimu kufundishia kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Nditiye amesema kuwa mradi huu ni mwendelezo wa kazi ya UCSAF kwa kupanua wigo wa mtandao wa intaneti mashuleni ili kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanatumia mtandao wa intaneti kusoma,
kupata maarifa na kujiendeleza “Leo tunazindua uunganishaji huu kwa shule kumi za sekondari za mkoa wa Simiyu ambazo zilipewa kompyuta hizo na UCSAF na Vodacom watakabidhi kompyuta mpakato mbili kwa kila shule pamoja na kifaa maalumu cha kuunganisha huduma ya intaneti kwa shule zote kumi,” amesema Nditiye.
Nditiye amewapongeza waalimu kwa kuwa wamekuwa wakikaa na wanafunzi kwa muda mrefu kwa siku nzima hata kwa wanafunzi wanaosoma shule za kutwa kuliko hata sisi wazazi “Niwaombe waalimu mtumie vifaa hivi kufundishia wanafunzi nanyi waalimu kujifunza badala ya kuviweka kwa kuogopa vinapata vumbi, mvitunze ili visiharibike kwa kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kununua,” amesisitiza Nditiye.
Vile vile, ametoa rai kwa kampuni nyingine za simu za mkononi kutoa vifaa vya TEHAMA kwa shule ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya intaneti ili waweze kujifunza.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema kuwa kompyuta zilizogawiwa hazitakaa stoo, zitatumika na kompyuta hizo zitakuwa enki ya mitihani yote na itawezesha wanafunzi wa mkoa kufaulu a wanufaike na intaneti na TEHAMA “Tuna amini kuwa kila halmashauri kuna Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano nah ii itatusaidia kwa wanafunzi wetu kupata mafunzo kwa kuwa tayari nchi ipo kwenye kiganja na tuna intaneti ya Vodacom ambayo tutaitumia bure kwa mwaka mmoja” amesema Mtaka Naye Mbunge wa Maswa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameishukuru UCSAF kwa kuupatia Mkoa wa Simiyu kompyuta 100 ili wanafunzi waweze kusoma kwa njia ya mtandao ambapo itawaongezea kiwango cha ufaulu.
“Tumeona juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kusema elimu bure zinasaidia watoto wetu kufaulu, nawapongeza waalimu, mnakaa na watoto wetu, kazi yenu ni ya wito, mnawajua watoto wetu, mimi ni motto wa mwalimu na mjukuu wa mwalimu, watoto wetu tukiwafundisha vizuri TEHAMA tutawapeleka mbele zaidi, na dunia ya sasa ni tofauti na wakati wetu tuliosoma, hivyo mna mazingira mazuri nah ii ni fursa ya ninyi kusoma zaidi,” amesisitiza Nyongo.
Akizungumza kabla hajakabidhi kompyuta mpakato 20 na vifaa vya kuunganisha intaneti kwa shule za sekondari 10 mkoani humo, Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, Roselyn Mworia amesema kuwa Vodacom imetengeneza tovuti ambayo itawasaidia kujifunza zaidi ili wanafunzi waweze kufaulu kwa kuwa ina masomo tofauti na mitaala tofauti na tovuti hii ni bure itawasaidia kusoma na kufanya marejeo ya masomo yao.
Naye mwalimu wa shule ya sekondari ya Mkodilana mkoani humo, Joseph Kazimoto amesema kuwa wanamshukuru Mkuu wa Mkoa wao, Mataka kwa kuanzisha kambi ya kuwakusanya wanafunzi kutoka shule mbali mbali mkoani humo na huduma ya intaneti itawawezesha kuongeza ufaulu na wana amini watashika namba moja kitaifa kwa kuwa mwaka jana walishika nafasi ya tisa kitaifa kwa matokeo ya kidato cha nne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Meatu, Daudi Mussa amemshukuru Mataka na wageni waliofika shuleni kwa kuwa wamehamasika kusoma na kufaulu zaidi na wameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kuwaweka kambi wanafunzi wote wa mkoa huo kwa kuwa wanawasaidia kuandaa maisha yao na kupata mbinu za kujibu maswali na sio kukariri.
Huduma hiyo ya mtandao wa intaneti imetolewa na kampuni ya Vodacom kwa muda wa mwaka mmoja kwa kuzipatia shule za sekondari kumi za Mkoa wa Simiyu kifaa maalumu cha kutoa huduma hiyo kwenye shule hizo. Shule za sekondari ambazo kompyuta zake zitaunganishwa kwenye huduma ya intaneti ni shule ya sekondari ya Simiyu, Maswa, Dutwa, Binzwa, Anthony Mtaka, Meatu, Nasa, Mwandoya, Itilima na Kanadi.
No comments:
Post a Comment