Ubalozi wa Nchi
za Falme za Kiarabu UAE umeendelea kuunga mkono kampeni ya Upasuaji wa
Moyo kwa Watoto kutoka familia duni Iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.
Paul Makonda ambapo leo October 31 wamemkabidhi hundi ya Shilingi
Milioni 27 kwaajili ya Bima za Afya kwa Watoto 500 wenye Tatizo la Moyo.
RC
Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha Watoto 500 wakiwemo
yatima na Wanaotokea familia duni Waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete kupata Bima za Afya zitakazowawezesha kupata Matibabu Bure kwa
kipindi cha Mwaka Mzima.
Aidha
RC Makonda amesema uamuzi wa kuwatafutia Bima za Afya umekuja baada ya
kubaini Watoto wengi wanaofanyiwa upasuaji wanahitajika kwenda Clinic
kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya Afya na Dawa lakini kutokana ugumu
wa maisha wanashindwa kumudu gharama jambo linalowafanya Wazazi au
Walezi wao kuuza Mali walizochuma kwa muda mrefu ili wapate fedha na
mwisho wa siku familia inazidi kuwa maskini.
Pamoja
na hayo RC Makonda amemshukuru Balozi kwa kuendelea kumuunga mkono
katika mambo mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto 100 wa kike kidato cha
tano na sita, Kumpatia madaktari bingwa wa Moyo Waliofanya upasuaji kwa
watoto 60, Kumsaidia futari kwaajili ya Maimamu wa Misikiti 800 huku
akitoa wito kwa Wananchi kuwa na moyo wa upendo wa kusaidia wenye
uhitaji.
Kwa upande wake
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Bw. Khalifa Abdulrahman Almarzooqi
amesema kuwa Ubalozi huo unafurahishwa na kazi nzuri ya RC Makonda
katika kusaidia Wananchi wenye uhitaji ndio maana wameamua kushirikiana
nae kwa kila jambo kwakuwa kila msaada anaoupokea unawafikia walengwa.
No comments:
Post a Comment